Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF yampa Arajiga ngoma ya Waarabu

Muktasari:

  • Mechi hiyo ya kundi D, itakayopigwa Novemba 29, 2026, Stade du 5 Juillet, mjini, Algiers, Algeria, Arajiga mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), amekabidhiwa jukumu hilo na kuzidi kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua mwamuzi raia wa Tanzania, Ahmed Arajiga kuchezesha mechi ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika itakayoikutanisha USM Alger ya Algeria dhidi ya AS Real de Bamako ya Mali.

Mechi hiyo ya kundi D, itakayopigwa Novemba 29, 2026, Stade du 5 Juillet, mjini, Algiers, Algeria, Arajiga mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), amekabidhiwa jukumu hilo na kuzidi kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania.

Arajiga mwenye uzoefu mkubwa baada ya kuchezesha hivi karibuni mechi ya Kariakoo Derby ambayo Simba ilishinda mabao 2-1, dhidi ya Yanga, kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini, Dar es Salaam, Oktoba 10, 2026, ameendelea kung’ara upande wa kimataifa.

Katika mechi hiyo ya Novemba 29, 2026, Arajiga atasimamia kati, huku kwa upande wa Video Assistant Referee yaani (VAR), Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua mwamuzi kutoka Zimbabwe, Brighton Chimene kusimamia teknolojia hiyo. Arajiga mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ni miongoni mwa waamuzi 35, walioteuliwa na CAF kwa lengo la kupata mafunzo mazuri ya kujiandaa na mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Mafunzo hayo yalianza rasmi kuanzia Novemba 18 hadi Novemba 23, ikiwa na lengo la kuwaandaa waamuzi hao kabla ya kuanza kwa kuchezwa mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa msimu wa 2026-2027. Arajiga ni mwamuzi pekee wa Tanzania aliyechaguliwa katika mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 18 hadi Novemba 23, kwa ajili ya kuweka kambi jijini, Cairo, Misri, ambapo amepata nafasi ya kuchezesha mechi hiyo ya USM Alger na AS Real de Bamako.