Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkomola anukia Bongo

STRAIKA Yohana Mkomola anayekipiga katika klabu ya Vorskla Poltava ya nchini Ukraine anatajwa yupo mbioni kujiunga na timu za Ligi Kuu kwa mkopo.

Mkomola yupo nchini baada ya vita zinazoendelea nchini Ukraine na sasa anadaiwa tayari ameanza mazungumzo na baadhi ya timu ili kukamilisha dili la kucheza kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Mmoja wa marafiki wa karibu na mchezaji huyo alilidokeza Mwanaspoti kuwa Mkomola kwa sasa anafikiria kucheza kwa mkopo nyumbani kisha ndio ajue mambo mengine.

"Kiukweli hajafikilia kwanza kurudi kule kwa sababu ya mazingira namna yalivyo ambayo yalimfanya arudi nyumbani, anataka acheze kwa mkopo hapa kisha aangalie mazingira mengine."

Ikumbukwe, FIFA wamewapa ruksa wachezaji wote wa Ukraine kujiunga na timu wanayoitaka ili kulinda vipaji vyao wakati wakisubili masuala ya usalama yakae sawa.

Mkomola mwenye umri wa miaka 22 alicheza Kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17 mwaka 2017 nchini Gabon.