Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkataba wa Bacca, Yanga kiboko

BACCA Pict

Muktasari:

  • Kuna taarifa za Simba ilikuwa inafukuzia saini yake, baada ya kugundua Bacca alikuwa amemaliza mkataba, kabla Wanamsimbazi hawajakamilisha hilo Yanga ilishtuka, ikatumia ushawishi wa nguvu ya pesa kumbakiza.

YANGA imefanya maboresho makubwa kwenye mkataba mpya wa beki Ibrahim Hamad ‘Bacca’, yaliyozingatia masilahi mapema ya mchezaji huyo, huku nyuma ya pazia ikitajwa Simba kuwa chanzo.

Kuna taarifa za Simba ilikuwa inafukuzia saini yake, baada ya kugundua Bacca alikuwa amemaliza mkataba, kabla Wanamsimbazi hawajakamilisha hilo Yanga ilishtuka, ikatumia ushawishi wa nguvu ya pesa kumbakiza.

Kuhusu kutakiwa Simba, kigogo mmoja wa klabu hiyo amesema baada ya kujua Bacca hana mkataba walipeleka ofa nono, ilizingatia kipengele cha mshahara wake wa kila mwezi na endapo kama Yanga isingeshtuka mapema katika hilo basi ingekuwa inaongelewa stori nyingine.

“Endapo kama usajili wake ungefanikiwa basi Simba angelipwa mshahara wa kila mwezi wa Sh30 milioni, kabla ya kufanya naye mazungumzo tulifahamu mkataba wake umemalizika hivyo hakukuwa na ubaya wowote kuhitaji huduma yake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Mchezaji akitumika kwa muda mrefu iwe Simba au Yanga, siyo rahisi kuondoka hasa pale timu inayommiliki ikiwa bado inahitaji huduma yake, hicho ndicho kilichotokea kwa Bacca, Yanga ilipogundua anaweza akaondoka tena kwenda Simba ikapambana kumbakiza na ilikuwa na nguvu hiyo na katika mpira wa miguu hilo ni kawaida.”

Mbali na hilo, rafiki wa karibu na Bacca amesema mkataba wake mpya wa miaka miwili aliyosaini umefanyiwa maboresho makubwa ya masilahi, tofauti na mwanzo.

“Dau lake la usajili ni zaidi ya Sh300 milioni, mshahara ni zaidi ya Sh20 milioni, mchezaji anapotoka timu moja kwenda nyingine kikubwa ni masilahi, hivyo kuhusu Simba kumtaka ni jambo la kweli na masilahi yao yalikuwa makubwa na ukizingatia maisha ya mpira kwa mchezaji siyo ya muda mrefu sana, hivyo anapopata fursa ya kutengeneza pesa lazima aitumie vyema”.

Ukiachana na Simba kuhitaji huduma yake kwa nje iliwahi kuhusishwa Raja Casablanca ya Morocco, kupeleka ofa mezani ya kumtaka Bacca, lakini haikufanikiwa kumsajili.

Kwa mara ya kwanza Bacca alijiunga na Yanga 2022 akitokea KMKM ya Zanzibar, kabla ya hapo nyingine alizowahi kuzichezea ni Jang’ombe Boys  (2017–2019), Malindi (2019–2021) pia alianza kuichezea Taifa Stars mwaka 2023 na  Zanzibar Heroes 2017.