Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miroshi amfunika Samatta

MIROSHI Pict

Muktasari:

  • Miroshi anakadiriwa kuwa na thamani ya Euro5.1 milioni, sawa na takriban Sh15.03 bilioni, akiongoza orodha hiyo mbele ya mshambuliaji Mbwana Samatta anayeichezea Le Havre ya Ufaransa.

KIUNGO wa Goztepe ya Uturuki, Novatus Miroshi, ndiye Mtanzania mwenye thamani kubwa zaidi ya soko miongoni mwa wachezaji wanaocheza nje ya nchi, kwa mujibu wa makadirio yaliyotolewa na mitandao ya FotMob na FootballTransfers.

Miroshi anakadiriwa kuwa na thamani ya Euro5.1 milioni, sawa na takriban Sh15.03 bilioni, akiongoza orodha hiyo mbele ya mshambuliaji Mbwana Samatta anayeichezea Le Havre ya Ufaransa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, thamani ya wachezaji huzingatia vigezo mbalimbali, vikiwamo ubora na hadhi ya ligi wanazoshiriki, umri wa mchezaji, uwezekano wa kuuzwa tena, dakika anazocheza, mchango wake uwanjani, muda uliosalia kwenye mkataba na uzoefu wa kimataifa, ikiwamo kuitumikia timu ya taifa.

SAMATTA Pict

Samatta anashika nafasi ya pili kwa makadirio ya Euro3.1 milioni, huku kiungo huyo akifuatwa na mshambuliaji chipukizi Cyprian Kachwele wa FC Kryvbas Kryvyi Rih ya Ukraine, anayekadiriwa kuwa na thamani ya Euro 560,000, sawa na Sh 1.65bilioni.

Wachezaji wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni Kelvin Pius John wa AaBorg ya Denmark, mwenye thamani inayokadiriwa kufikia Euro 410,000, sawa na Sh1.21 bilioni, na Haji Mnoga wa Patro Eisden, anayekadiriwa kuwa na Euro 365,000, sawa na Sh1.08 bilioni.

Alphonce Msanga wa JS Kabylie ya Algeria anakamilisha orodha hiyo kwa makadirio ya Euro 345,000, sawa na Sh1.02 bilioni.

MIROSHI Pict

Kinachojitokeza katika orodha hiyo ni uwepo wa wachezaji wengi vijana. Ukimtoa Samatta mwenye umri wa miaka 33, wengine watano wana umri wa kati ya miaka 21 na 24, hali inayowaacha na nafasi ya kuendelea kukuza uwezo wao na kuongeza thamani katika soko la usajili.

Uongozi wa Miroshi kwenye orodha hiyo unaonyesha tofauti ya makadirio ya thamani yake na wachezaji wengine, huku umri wake, kiwango cha ushindani wa ligi anayoichezea na mchango wake uwanjani vikiwa miongoni mwa vigezo vinavyoweza kuathiri thamani hiyo.