Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miroshi kazi ipo leo Uturuki

MIROSHI Pict

Muktasari:

  • Ushindi kwa Goztepe unaweza kuwa mwanzo wa kurejesha hali ya kujiamini na kuipa timu nafasi ya kupanda kwenye msimamo, lakini matokeo mengine mabaya yataendeleza presha kwa kikosi hicho.

CHAMA la Mtanzania, Novatus Miroshi, Goztepe, lina kibarua kizito leo Oktoba 12 litakaposhuka dimbani kuvaana na Eyupspor katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki, unaotarajiwa kuanza saa 2 usiku kwa saa za Tanzania, huku timu hizo zikiwa na changamoto ya kutafuta matokeo yatakayoziondoa kwenye nafasi za chini.

Mchezo huo unazikutanisha timu zinazofuatana kwenye msimamo wa ligi, Goztepe ikiwa nafasi ya 17 huku Eyupspor ikishika nafasi ya 18. Timu hizo zimekusanya pointi tatu kila moja katika mechi saba, hali inayoufanya mchezo huo kuwa muhimu kwa pande zote mbili katika harakati za kujiweka kwenye nafasi salama.

Miroshi na wenzake wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na presha ya kutafuta ushindi wa kwanza baada ya kuanza msimu kwa kusuasua.

Goztepe haijaonja ushindi katika mechi zake sita zilizopita, ikikusanya sare tatu na kupoteza tatu, mwenendo unaoifanya mechi ya leo kuwa kipimo muhimu cha uwezo wao wa kurejea kwenye ushindani.

MIRO 01

Hali hiyo ni tofauti na matarajio yaliyokuwepo kutokana na mwenendo wa timu hiyo msimu uliopita na ilipambana katika nafasi za juu na kuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikiwania nafasi nne za juu.

Nyota huyo amekuwa msaada kwenye kikosi hicho huu ukiwa msimu wake tatu mfululizo ambapo alisajliwa msimu wa 2024/25 akitokea Zulte Waregem ya Ubelgiji.

Ushindi kwa Goztepe unaweza kuwa mwanzo wa kurejesha hali ya kujiamini na kuipa timu nafasi ya kupanda kwenye msimamo, lakini matokeo mengine mabaya yataendeleza presha kwa kikosi hicho.