Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama la Samatta hali tete Ufaransa

SAMATTA Pict

Muktasari:

  • Kabla ya michezo ya raundi ya 11, Le Havre ilikuwa timu pekee ambayo haikuwa imeonja ushindi baada ya klabu nyingine kucheza mechi 10 za ligi. Hali hiyo imezidi kuwa mbaya baada ya kupoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Troyes, Novemba 20, matokeo yaliyoiacha ikiwa na pointi mbili pekee kutokana na sare mbili na vipigo tisa.

LICHA ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, kuendelea kupambana na kutoa mchango wake katika safu ya ushambuliaji, klabu yake ya Le Havre inakabiliwa na wakati mgumu katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), ikiwa mkiani mwa msimamo bila kupata ushindi katika mechi 11 ilizocheza msimu huu.

Kabla ya michezo ya raundi ya 11, Le Havre ilikuwa timu pekee ambayo haikuwa imeonja ushindi baada ya klabu nyingine kucheza mechi 10 za ligi. Hali hiyo imezidi kuwa mbaya baada ya kupoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Troyes, Novemba 20, matokeo yaliyoiacha ikiwa na pointi mbili pekee kutokana na sare mbili na vipigo tisa.

Samatta amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi ya kuongoza safu ya ushambuliaji ya Le Havre. Takwimu za Opta zinaonyesha kuwa kabla ya mchezo dhidi ya Troyes, mshambuliaji huyo alikuwa amecheza mechi zote 10 za ligi, akianza tisa na moja akitokea benchi, huku akikusanya dakika 742 na kufunga mabao mawili.

Mabao hayo aliyafunga katika michezo tofauti. La kwanza lilikuwa Agosti 29 dhidi ya Olympique Lyonnais katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, kabla ya kuongeza jingine Septemba 19 dhidi ya Toulouse, ingawa Le Havre ilipoteza kwa mabao 3-2.

SAMA 02

Hivyo, katika pointi mbili ambazo Le Havre imekusanya hadi sasa, Samatta amekuwa sehemu ya mchango uliowezesha timu hiyo kupata moja kupitia sare dhidi ya Lyon.

Katika mchezo dhidi ya Troyes, Samatta aliendelea kuwa sehemu ya mipango ya timu hiyo licha ya kupata muda mfupi wa kucheza. Aliingia dakika ya 86 akichukua nafasi ya Josh Maja, kabla ya kujaribu kupiga shuti dakika ya 90, lakini lilizuiwa na mabeki wa wapinzani.

Kwa upande wa uzalishaji wa mabao, Le Havre imekuwa na changamoto katika safu zote mbili, ikiwa imefunga mabao 10 na kuruhusu 25 katika mechi 11 ilizocheza, tofauti ya mabao 15.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, wakati akishangilia moja ya bao katikia mechi ya Ligi Kuu Ufaransa. Picha na Mtandao

Takwimu hizo zinaonyesha ukubwa wa kazi inayokikabili kikosi hicho, ambacho kinahitaji kuboresha umaliziaji wa nafasi za kufunga na kuimarisha safu ya ulinzi ili kuanza kujinasua kutoka nafasi ya mwisho kwenye msimamo.

Msimu uliopita, Samatta alicheza mechi 27 akiwa na Le Havre, akifunga mabao mawili na kutoa asisti moja.

Hata hivyo, pamoja na matokeo yasiyoridhisha, klabu hiyo imefanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwa kumuondoa Didier Digard na kumteua Valérien Ismaël kuwa kocha mkuu kuanzia Novemba 12.

Mabadiliko hayo hayajamwondoa Samatta kwenye mipango ya timu, kwani mshambuliaji huyo ameendelea kupata nafasi chini ya kocha huyo mpya, huku Le Havre ikihitaji matokeo mazuri ili kubadili mwelekeo wa msimu wake.