Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miloud Hamdi: Sasa Simba waje tu

YANGA Pict

Muktasari:

  • Awali Yanga iliondoa ratiba ya maandalizi ya mchezo huo kwa benchi lao la ufundi na wikiendi iliyopita ratiba hiyo ikarudishwa na kocha Hamdi akafunguka kila kitu na namna alivyoanza mipango ya kujiandaa na pambano hilo la Ligi Kuu Bara litakaloamua bingwa wa msimu huu.

YANGA kazi imerudi, kwani kama unakumbuka kocha wa timu hiyo, Miloud Hamdi alitamka hana ratiba na mchezo wa dabi dhidi ya Simba, lakini sasa amefungua faili la mechi hiyo, akisema ameshajulishwa juu ya uwepo wa mchezo na yupo tayari kuvaana na watani wa jadi hao hiyo Juni 25.

Awali Yanga iliondoa ratiba ya maandalizi ya mchezo huo kwa benchi lao la ufundi na wikiendi iliyopita ratiba hiyo ikarudishwa na kocha Hamdi akafunguka kila kitu na namna alivyoanza mipango ya kujiandaa na pambano hilo la Ligi Kuu Bara litakaloamua bingwa wa msimu huu.


Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Hamdi alisema ameshapata taarifa kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo juu ya mechi hiyo na kusisitiza kikosi hicho kipo tayari kupigania ushindi Uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 25 akiamini ndiyo ulioshikilia hatma ya kutetea taji kwa msimu wa nne.

Hamdi alisema kikosi hicho kipo tayari sasa kwa michezo minne ya kumalizia msimu, mitatu ya ligi na mmoja wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Singida Black Stars utakaopigwa Juni 28.

Kocha huyo alisema hata wachezaji wa timu hiyo, aliwakuta wana hamu na mchezo huo na wakati wa maandalizi yake ukifika watajipanga kwenda kushinda.

“Tunaziheshimu timu zote, hapo kabla hatukuwa na ratiba na mechi dhidi ya Simba, lakini naona sasa mambo yamekuwa, sasa tupo tayari kwa mchezo huo na tutahitaji kushinda kama tulivyoshinda mechi zingine.

“Unajua Yanga ndiyo timu pekee ambayo imezifunga timu zote msimu huu angalau kwa mchezo mmoja, unapoona rekodi kama hii unapata tafsiri sahihi ya ubora wa kikosi chetu, tunataka kushinda mechi zote zilizosalia.


KAMBI YA DABI ZENJI

Rasmi Yanga itacheza mchezo wa nyumbani dhidi ya Dodoma Jiji, Juni 22 visiwani Zanzibar kwenye Uwanja wa New Amaan Complex na sasa kambi ya Dabi pia itafanyika huko huko kisha ya kuja jijini Dar es Salaam siku moja kabla ya pambano hilo litakalokuwa la 114 katika Ligi ya Bara tangu 1965.

Taarifa kutoka kwa mabosi wa Yanga ni kwamba mara baada ya timu hiyo kumaliza mchezo wa Dodoma kikosi hicho kitabaki visiwani humo kujiandaa kwa mechi hiyo dhidi  Simba itakayopigwa Juni 25 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tutacheza na Dodoma huko na baada ya hapo hatutarudi hapa Dar es Salaam mpaka tutakapocheza dhidi ya Simba, tunataka kushinda mechi ya Simba ili kunogesha sherehe zetu za ubingwa wa 31 lakini ukiwa ubingwa wetu wan ne mfululizo,” alisema bosi mmoja wa juu ndani ya Yanga.