Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka 10 Bayern imetwaa nusu ya mataji ya Ligi Kuu

TOLEO lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, Mwandishi Marti Perarnau aliendelea na mahojiano yake na Mwenyekiti wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge na safari hii mwenyekiti huyo alielezea furaha aliyokuwa nayo baada ya Pep kuwa kocha wa Bayern. Sasa endelea…

“Ni wazi katika hilo ukiingiza mechi yetu na Real Madrid kidogo inaleta utofauti katika uchambuzi lakini pia ni muhimu kwangu kuangalia namna tulivyocheza mechi yetu na Man City na Man United pamoja na mechi yetu na Arsenal jijini London na ile mechi yetu ya Bernabeu dhidi ya Real Madrid.

“Yote hayo pia ni muhimu, tunahitaji kuwa na uwiano sahihi katika mambo haya, nina furaha kuwa na Pep akiwa ndiye kocha wetu, ana kipaji cha aina yake, naweza kuelewa ni kwa nini hasa alikuwa mnyonge baada ya mechi yetu na Real Madrid lakini bado anabaki kuwa kocha wa kiwango cha juu, juu zaidi.

Perarnau alimuuliza Rummennige: “Mwaka 2015 fainali ya Ligi ya Mabingwa inachezwa (ilichezwa) Ujerumani jijini Berlin, je, na hilo nalo ni lengo lenu muhimu kama ilivyo Bundesliga?

Rummenigge: “Ni kweli taji muhimu zaidi katika msimu wowote ni la ligi, popote pale, utatakiwa kucheza mechi 34 katika Bundesliga, kwa hiyo ushindi wake unadhihirisha ubora wako, kutokana na hadhi ya soka la zama hizi unaweza kuwa na siku moja tu mbaya na kujikuta uko nje ya Ligi ya Mabingwa.

“Hicho ndicho kilichojitokeza, katika ligi unaweza kupoteza mechi kwa mabao 4-0 lakini kesho ukijipanga na kuja vizuri unaweza kushinda mechi nyingine 10 zinazofuata lakini Ligi ya Mabingwa ni tofauti, ni kukabana koo na pengine ndio ushindani mkali wa taji lakini muhimu ya yote ni taji la ligi litabaki kuwa na umuhimu wake. Mwandishi Perarnau alimuuliza tena Rummenigge: “Bayern inatakiwa kuchukua uamuzi, kama ni kuendelea na timu ileile ambayo imeshinda kila kitu na imeendelea kushinda au kuingiza damu changa?

Rummennige: “Tunahitaji kuwa wazi katika mabadiliko yoyote tunayoyafanya, inahitaji umakini Sammer (Matthias) ambaye ni mkurugenzi wetu wa michezo, kocha pamoja na mimi wakati wowote huwa tunajaribu kufikia mwafaka.

“Tunatakiwa kufahamu ukweli kuhusu uwezo wa kifedha wa timu na kuendelea na mambo mengine kwa tahadhari, itakuwa ni upuuzi kuruhusu mawazo yetu na uamuzi tutakaoufanya utokane na kufungwa katika mechi yetu ya hivi karibuni.

“Kama ungeniuliza swali hilo wiki tano zilizopita ningekwambia tuna mambo madogo madogo ya kubadili kwa sababu timu ilikuwa ikifanya kazi vizuri, tumeshinda taji la ligi kwa staili ya kuvunja rekodi, tulikuwa katika mbio za kutetea taji letu la Ligi ya Mabingwa na tulikuwa katika fainali ya Kombe la Ujerumani.

“Kwa sasa baada ya kipigo hiki (dhidi ya Real Madrid) kidogo mambo yamebadilika, lakini wakati wote nimekuwa nikiamini mambo yanapokwenda kombo ni vizuri kwenda nyumbani, kulala ukilifikiria hilo na baadaye unarudi kwa lengo la kuweka mambo yako sawa taratibu na mkiwa pamoja.

Perarnau: Ni wazi usajili wa Robert Lewandowski hauwezi kutosha, unahitaji usajili wa mchezaji mwingine wa kiwango cha juu, usajili ambao utaimarisha hadhi ya Bayern na kuwa tishio kwa yeyote anayejitokeza hasa kwa hapa hapa Ujerumani?

Rummennige: Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Bayern imetwaa nusu ya mataji yote ya ligi, na ni wazi kumekuwa na mataji mengine, Dortmund imeshinda mara mbili, Wolfsburg nayo imeshinda kama ilivyo kwa Stuttgart, timu ambayo baadaye ikawa yenye kupambana kujinasua kushuka daraja.

“Bayern ni klabu yenye nguvu, na tumefanya juhudi kuimarisha uimara wetu kwa kila namna, tuna mfumo ulio imara wa fedha ambao kupitia huo tumeendeleza mambo yetu na hapo hapo tutaweza kufanya usajili wa maana.”

Itaendelea Jumamosi ijayo…