Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfaransa amchenjia Mwambusi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

YANGA imerudi upya mezani kuanza upya mchakato wa Kocha Mkuu Mpya baada ya kuzinguana na Mfaransa Sebastian Migne na sasa wakati wowote kuanzia leo watamshusha mwingine mpya anayekuja na jeshi lake kamili.

YANGA imerudi upya mezani kuanza upya mchakato wa Kocha Mkuu Mpya baada ya kuzinguana na Mfaransa Sebastian Migne na sasa wakati wowote kuanzia leo watamshusha mwingine mpya anayekuja na jeshi lake kamili.

Dili la Migne limeyeyuka ghafla baada ya kupishana katika hatua za mwisho juu ya uundwaji wa benchi lake, akimchenjia kocha wa sasa Juma Mwambusi sambamba na kipengele kimoja cha malipo yake.

“Migne amekuwa na vipengele vingi tukimtumia mkataba anataka hiki mara hiki hataki, sasa tumeona tunatumia muda mrefu kukubaliana naye tu kitu ambacho huku kwetu kinatumaliza,” alisema mmoja wa mabosi ambaye jina lake limehifadhiwa.

Huku taarifa, zikiongeza Mfaransa huyo alitaka makocha waliopo sasa akiwamo Mwambusi na yule wa makipa Razack Siwa, waondolewe ili aje na watu wake.

Hata hivyo, makocha hao tayari wameingia mkataba hivi karibuni na kama wakiondolewa ni sawa na kuvunjiwa mikataba na hivyo kuilazimisha klabu kuwalipa fidia, kitu ambacho mabosi wameshtuka na kuona wataingizwa mkenge, wakati hivi karibuni tu waliachana na makocha Zlatko Krmpotic na Cedric Kaze na wasaidizi wao kabla mikataba yao haijaisha.

Awali tayari alishawajulisha wachezaji kwa njia ya simu anakuja, lakini ghafla juzi aliwapigia tena simu na kuwataarifu huenda asije baada ya mambo kutibuka.

Habari zaidi, zinasema juzi mchana mabosi wa Kamati ya Ufundi wa Yanga ghafla walirudi mezani kuanza upya mchakato huo kutafuta mtu wa haraka anayekuja kuchukua majukumu hayo wakikaa kwa pamoja na mabosi wa juu wakiwemo Senzo Mazingisa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said.

Mmoja wa viongozi wa juu Yanga (jina kapuni) alilihakikishia Mwanaspoti kocha huyo anakuja Jumatatu na moja kwa moja atasaini mkataba wa kufanya nao kazi. Hata hivyo, alikataa kabisa kutaja jina, akidai wanataka kuwasapraizi mashabiki wao.

“Makubaliano ya awali yameshafanyika na kilichobaki ni yeye kuja kusaini mkataba na kuendelea na kazi, atamalizia msimu na kuendelea nasi msimu ujao.”

Kiongozi huyo aliongeza, kocha huyo anayetokea Ulaya, atakuja na msaidizi wake ambaye sio Mtanzania na atakuwa anasaidiana na Mwambusi.

“Kocha Mkuu anakuja na msaidizi wake, atakuwa pamoja na Mwambusi mpaka mwisho wa msimu, kisha tutaangalia itakavyokuwa.”

Yanga itashuka uwanjani kwa mara nyingine Aprili 20 dhidi ya Gwambina kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1:00 usiku, kabla ya kuvaana na Azam FC Aprili 25 na kusafiri hadi mjini Sumbawanga kumalizana na Tanzania Prisons katika mechi ya 16 Bora ya ASFC.