Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi ainasa rekodi ya Ronaldo de Lima

Muktasari:

Messi hashikiki, Desemba 19, 2009, hatimaye Barcelona ikashinda taji lake la kwanza la klabu la dunia baada ya kukaribia kufanya hivyo mwaka 1992 na 2006 wakati huo likijulikana kwa jina la taji la Mabara.

TOLEO lililopita, mwandishi Luca Caioli alizungumzia mechi ya mwisho ya Ronaldo akiwa na Man United katika msimu wa 2008/09 kabla ya kuhamia Real Madrid pamoja na mchezaji huyo kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia huku wakati Messi alishika nafasi ya pili katika tuzo hiyo. Endelea…

Tofauti na msimu uliopita, Messi wa msimu huu wa 2008/09 hakuandamwa na janga la majeraha katika mechi zote 51 alizocheza.

“Ulikuwa mwaka wa kipekee, nimeufurahia wote,’’ alisema Messi ambaye kubwa jingine alilovuna wakati huo ni kushika nafasi ya pili katika tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa dunia nyuma ya Ronaldo lakini miezi 12 baadaye alimbwaga Ronaldo na kutwaa tuzo hiyo.

2009/10

Messi hashikiki, Desemba 19, 2009, hatimaye Barcelona ikashinda taji lake la kwanza la klabu la dunia baada ya kukaribia kufanya hivyo mwaka 1992 na 2006 wakati huo likijulikana kwa jina la taji la Mabara.

Hadi kubeba taji hilo waliifunga Estudiantes de La Plata na Messi alifunga bao, ni baada ya kumzidi ujanja staa mwenzake wa Argentina, Juan Sebastian Veron na kuitumia vizuri krosi ya Dani Alves kuujaza mpira wavuni dakika ya 110.

Kilichowafurahisha wengi ni kwamba Messi alifunga bao hilo kwa kuunganisha krosi hiyo kwa kifua katika mazingira ambayo hakuna aliyetarajia na hatimaye ubao ukasomeka 2-1 na filimbi ya mwisho ikapulizwa, Barca wakatangazwa vinara wa klabu bingwa ya dunia.

Pia, walikuwa ndio vinara wa ligi ya mabingwa, Super Cup Ulaya, Super Cup Hispania, Kombe la Mfalme na La Liga, Na kama hiyo haitoshi, Messi akavunja rekodi nyingine, Januari 16, 2010 katika mechi ya La Liga dhidi ya Sevilla kwa kuwa mchezaji mwenye umri mdogo wa Barcelona kufunga mabao 100, alikuwa ndio kwanza ana miaka 22 na miezi sita.

Miezi mitatu baadaye akawa mchezaji wa kwanza wa Barca kufunga mabao manne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuilaza Arsenal kwa mabao 4-1 katika mechi ya pili ya robo fainali ya michuano hiyo.

Hadi mwisho wa msimu akawa na mabao 46 katika mashindano yote, kati ya mabao hayo zimo hat trick nne pamoja na mabao 34 aliyoyafunga katika La Liga na hivyo kuifikia rekodi ya staa wa Brazil, Ronaldo de lima aliyefunga mabao kama hayo katika msimu wa 1996/97 wakati huo akiichezea Barcelona.

Messi akawa amezifunika rekodi zote alizokuwa nazo tangu ajiunge Barcelona misimu takriban sita iliyopita ingawa kwa kipindi hicho pigo pekee kwa Messi ilikuwa ni kutolewa kwao katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Inter Milan wakati huo ikinolewa na Jose Mourinho ambayo ndiyo iliyotwaa taji la ligi hiyo.

Kwa Ronaldo msimu ulikuwa na mengi mazuri ya kuvutia, lakini hilo halikuwa kwa sababu ya kiwango chake cha uchezaji kwani alianza kwa moto, bora kati ya yote ni mabao saba aliyofunga katika mechi tano za mwanzo.

Hadi mwisho wa msimu akawa amefunga jumla ya mabao 33 licha ya kupata majeraha na kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili. Alifunga mabao 26 katika La Liga ikiwamo hat trick yake ya kwanza ya La liga katika mechi ya Real Madrid dhidi ya Mallorca iliyochezwa Mei, 5, 2010 pamoja na mabao saba katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ronaldo alikuwa burudani kwa mashabiki wa Real Madrid, lakini pia alikuwa na wakati wa kuchukizwa na mambo, Real ilikuwa na msimu wa hovyo, katika ligi ya mabingwa iliishia hatua ya 16 bora, katika Kombe la Mfalme nako hali haikuwa vizuri na La Liga ilitawaliwa na Barcelona.

Itaendelea Jumanne…