Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchezo wa kubahatisha wampa bodaboda

Mkazi wa Ruvuma, James Chiwangu ameibuka mshindi wa mwezi katika droo ya Kopa Tukubusti ya inayoendelea nchini.
Katika droo hiyo inayoendeshwa na benki ya Letshego Faidika, Chiwangu ameibuka mshindi wa jumla mwezi huu na kuzawadia pikipiki mpya aina ya boxer.

Akizungumzia ushindi wake, Chiwangu amesema ni faraja kwake, ukitokana mkopo wa Shilingi laki mbili aliopewa na benki hiyo.

“Najisikia fahari kubwa sana kushinda pilipiki kupitia mkopo wangu ambao ulinisaidia kwenye masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, wakati huo huo kuingia kwenye droo na kuibuka mshindi wa pikipiki katika kampeni hii,” amesema Chiwangu.

Mbali ya Chiwangu ambaye ni mfanyakazi wa Halmashauri ya mkoa wa Ruvuma, pia benki ya Letshego Faidika imetangaza washindi wengine wanne wa kampeni hiyo ambao kila mmoja amejishindia asilimia 50 ya mkopo aliopewa.

Washindi hao ni Ismail Lugenge, mkazi wa Liwale mkoa wa Lindi aliyeshinda sh 103,000 , Lutende Sospeter wa Kibondo, mkoani Kigoma ambaye ameshinda kiasi cha Sh100,000 na Joyce Mshana pia wa Kibondo aliyeshinda kiasi cha Sh228,034.

Pia katika orodha hiyo ni Ibrahim Jalala ambaye ameshinda kiasi cha sh925,772 kupitia droo hiyo na kufikisha jumla washindi 10 waliofadika na kampeni hiyo mpaka sasa.

Meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika, Asupya Nalingigwa aliwaomba wateja wao kuchangamkia mikopo yao ili kushinda zawadi mbalimbali na kuweza kusaidia kugharimia mahitaji mbalimbali.

Nalingigwa amesema bado washindi 20 ili kukamilisha kampeni hiyo itakayofikia tamati Desemba mwaka huu na kuwaomba wateja wao kuendelea kukopa na kuingia kwenye droo hiyo.

 “Tumeweka jumla ya Sh50 bilioni kwa ajili ya kukopesha wateja wetu. Mteja anaweza kushinda fedha ya ziada (Bonus) ya asilimia 50 ya kiasi cha fedha alichokopa kupitia kampeni hii mpya ya Kopa Tukubusti.

"Lengo hapa ni kubadili maisha ya wateja wetu na mtu mmoja anaweza kukopa hadi Sh150 milioni, mtu huyu akishinda kampeni ya Kopa Tukubusti, atazawadiwa Sh milioni 75,” amesema Nalingigwa.

Kwa mujibu wa Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.