Mbwa wawili wa Sanchez wavaa jezi za Man United
England. Ujio wa mchezaji mpya wa Manchester United, Alexis Sanchez umekuja na kasi mpya ya mauzo ya jezi yake, huku akianza kubadili rangi za vitu mbalimbali kuwa na muonekano nyekundu.
Picha zilizosambaa mtandaoni, zilionekana akiwa amewavalisha mbwa wake wawili Atom na Humber ambao walimetinga uzi mwekundu wa Man United.
Uhamisho wa mchezaji huyo ulikamilika juzi Jumatatu na jana aliambatana na mbwa wake kwenye Hoteli ya Lowry ambako ni makazi ya Jose Mourinho na wakati mwingine kikosi cha Man United hufikia hapo kabla ya mechi zao Uwanja wa Old Trafford.
Hoteli hiyo ndiko mazungumzo ya Sanchez na uongozi wa Man United yalikokuwa yanafanyika kumalizia mkataba wao.
Mchezaji huyo alituma kwenye ukurasa wake wa Istagram akiwaonyesha mbwa pamoja na mtoto wake waliovaa jezi za Man United.
Awali, alisema kwamba mbwa, marafiki zake wa karibu pamoja na watoto wake wataonekana wakiwa wamevaa jezi nyekundu.
Sanchez amekuwa mchezaji ghari anayelipwa kwenye Ligi Kuu England na tayari ameshaanza kubadili baadhi ya vitu kuonyesha kwamba amehamia Man United.