Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbulgaria afichua siri za Yanga

PANTEV Pict


YANGA ipo pale juu ya msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kufikisha pointi sita ambazo ni sawa na za Simba lakini zinatofautishwa na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, lakini kuna kocha mmoja wa kigeni ambaye alipita kwa Wekundu hao wa Msimbazi msimu uliopita akisema mabingwa watetezi wa ligi hiyo, wako siriazi sana na wanaweza kuja kumuaibisha mtu.


Kocha wa zamani wa Simba, Dimitar Pantev raia wa Bulgaria, ndiye aliyetoa kauli hiyo akisema Yanga mpango wao na namna wanavyoutekeleza kama wakikutana na timu ambayo haijashiba pumzi ya kutosha lazima ipoteze vibaya.


Pantev ambaye yupo hapa nchini akihudhuria mafunzo ya leseni ya CAF, amehudhuria mechi ya Yanga dhidi ya Coastal Union na kufuatilia zingine, akisema Yanga wachezaji wake wameshiba pumzi vizuri ambapo wana uwezo wa kukupa presha wakati wanashambulia, kisha wakabadili presha hiyo wakati hawana mpira kwenye kupokonya umiliki wa mchezo.

Kocha huyo ambaye wakati anaifundisha Simba mpaka anaondoka, hakuwahi kukutana na Yanga, amesema ubora huo wa viungo wa Yanga ndio ambao umezipa timu nyingi wakati mgumu kuwashambulia kwa nguvu mabingwa hao.

“Nimeangalia mechi za Yanga kuanzia ile wakati wanacheza na timu yangu ya zamani Simba, nimeangalia pia mechi zingine za timu zingine, Yanga wana timu nzuri sana, wana pumzi ya kutosha lakini ubora wao mkubwa upo kwenye eneo la kiungo,”€  amesema Pantev. “Wakati Yanga wanakushambulia, wanaweza kukupa presha kubwa ili ufanye makosa, sasa kama hauna pumzi ya kutosha wakati wowote utafanya makosa, ukiangalia Coastal Union walijitahidi sana lakini muda ulivyosogea wakajikuta pumzi yao inapungua.

“Ukiangalia utagundua kwenye mechi zao nyingi kipa wao ni kama amepumzika na hapati presha kubwa ya kushambuliwa, hii inatokana na ubora wa eneo la kati ambalo hata mabeki wao wanajikuta wanafanya kazi ndogo.”

Kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Yanga ilionyesha ubora mkubwa wa kuzima mashambulizi ya wapinzani na kujikuta Wekundu hao wanamaliza dakika 45 za kwanza bila ya kuwa na shuti lililolenga lango, huku wakifanikiwa hivyo zikibaki dakika kumi mechi kumalizika.

Hilo pia likaendelea kwenye mechi dhidi ya Namungo ambapo shuti pekee ambalo walipiga wenyeji hao likawapa bao lililofungwa na Helbert Lukindo.

Juzi wakati Yanga ikicheza dhidi ya Coastal Union, hilo pia likajirudia ambapo shuti pekee la mpira wa adhabu ndogo likipigwa na kiungo Gradi Kiala ndio lililoipa timu yake bao baada ya mpira kumgonga beki Chadrack Boka na kumpoteza kipa Djigui Diara.