Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbio za Pursuit kushika kasi Dar es Salaam

BAISKELI Pict

Muktasari:

  • Akitangaza zawadi hizo, mwanzilishi wa program ya Pursuit, Hilary Chuwa amesema zawadi zimegawanywa katika makundi matatu na zitakuwa kwa wanaume, wanawake na wakongwe huku pia zikitofautiana umbali.

MBIO za Baiskeli za Pursuit zimetaja zawadi kwa washindi wa makundi tofauti zitakazofanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 27,2026.

Akitangaza zawadi hizo, mwanzilishi wa program ya Pursuit, Hilary Chuwa amesema zawadi zimegawanywa katika makundi matatu na zitakuwa kwa wanaume, wanawake na wakongwe huku pia zikitofautiana umbali.

"Wanaume mbio zao zitakuwa na mizunguko sita ambazo zitakimbiwa kwa kilometa 102 na mshindi wa kwanza atapata Sh2.5 milioni, wa pili Sh1.5 milioni, wa tatu Sh1 milioni, wanne Sh700,000, wa tano Sh500,000, wa sita Sh400,000, wa saba Sh300,000, wa nane Sh250,000, wa tisa Sh200,000 na wa kumi Sh150,000,” amesema Chuwa.

Kundi la washiriki wanawake mshindi wa kwanza atajichukulia Sh1 milioni, wa pili Sh700,000, wa tatu Sh500,000, wa nne Sh300,000, wa tano Sh200,000.

Kwa upende wa wakongwe kutakuwa na washindi watatu pekee na wa kwanza atapata Sh500,000, wa pili Sh300,000 na wa tatu Sh200,000.

“Tunatoa wito kwa washiriki wote kuendelea kujiandaa kikamilifu, ushindani utakuwa mkubwa kutokana na namna zawadi hizi zilivyoboreshwa msimu huu.”