Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya City yaingia kimataifa

Mara baada ya pazia la Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2022-23 (TPL) pamoja na Ligi kuu ya Uingereza (EPL) kufunguliwa siku za hivi karibuni, Klabu ya Mbeya City, Chelsea, Aston Villa, Newcastle United pamoja na Leicester City zaingia kwenye udhamini mpya na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Parimatch inayoendesha shughuli zake nchini.


Hayo yamebainishwa na Ofisa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed na kusema  kwamba wamejipanga vilivyo katika kukuza na kuleta changamoto mpya kwenye soka la Tanzania kwa kuangalia katika kushirikisha vilabu vya ndani na nje ya nchi.


“Tunafuraha kubwa kutangaza kuwa washirika na Newcastle United, Leicester City, Aston Villa pamoja na Chelsea, uhusiano huu utakuwa muhimu kwa pande zote kwa namna moja ama nyingine. Hii imekuwa desturi yetu Parimatch kushirikiana na vilabu vikubwa vya soka duniani kama mtakumbuka vizuri huu ni muendelezo tu kwani tulishawahi kufanya kazi na vilabu hivi katika msimu uliopita, lakini pia tumekuwa wa kwanza kuweka historia kwa Tanzania kufanya hivyo”, amesema Ismael.


Ismael amesema Mbeya City itakuwa katika ‘level’ zingine ndani ya msimu huu licha ya kwamba, imepoteza mchezo wake mmoja muhimu ambao amecheza akiwa katika dimba la nyumbani la Sokoine dhidi ya Azam FC.


Mbeya City mechi ijayo Oktoba 14 itacheza dhidi ya Polisi Tanzania, Ismael amesema timu hiyo itaondoka na alama 3 kibindoni na kuanza kasi ya kutafuta ubingwa wa msimu huu, hakuna kinachoshindikana katika soka kila kitu ni jitihada na mbinu kali za kupambana na mpinzani.

Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni kwenye kasino na michezo ya virtual, Parimatch ipo zaidi ya nchi 15 duniani kote ikiwa na mamilioni ya wateja. Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye michezo, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match