Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya City yachangiwa Sh3 milioni kuifunga Kagera Sugar

Muktasari:

  • Fedha hizo zimetolewa leo Aprili 18, 2023 wakati wa Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Spika kwa wachezaji wa Mbeya City jijini Dodoma wakiwa safarini kuelekea Bukoba kwa ajili ya mechi itayochezwa uwanja wa Kaitaba.

Spika wa Bunge la Tanzania  Dk Tulia Ackson ametoa Sh2 milioni kwa timu ya Mbeya City ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya Kagera Sugar Aprili 23.

Fedha hizo zimetolewa leo Aprili 18, 2023 wakati wa Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Spika kwa wachezaji wa Mbeya City jijini Dodoma wakiwa safarini kuelekea Bukoba kwa ajili ya mechi itayochezwa uwanja wa Kaitaba.

Akikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Dk Tulia, mbunge Lupa Chunya  Masache Kasaka kwa kushirikiana na wabunge wa Mbeya nao wametoa  Sh1 milioni na kufanya jumla kuwa Sh3 milioni.

Pamoja na mambo mengine, wabunge hao wameahidi kununua ushindi kwa timu ya Mbeya City kwa kila mechi zilizosalia kwenye ligi Kuu ya Tanzania inayoendelea