Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayanga apata dawa Ligi Kuu

MAYANGA Pict

Muktasari:

  • Mbeya City ilianza vyema msimu kwa takribani mechi nne, kabla ya mambo kuwatibukia na kujikuta wakicheza michezo sita mfululizo bila ushindi na baadaye juzi kufufuka kuilaza Singida Black Stars bao 1-0.

BAADA ya ushindi wa mechi iliyopita, Mbeya City imesema inahitaji kuendeleza moto Ligi Kuu kuhakikisha inaondokana na presha ndani ya uwanja, huku ikiivimbia Namungo.

Hata hivyo, benchi la ufundi limepiga marufuku mastaa wake kupumzika kipindi hiki ligi ikiwa imesimama kupisha kalenda ya kimataifa kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika (AFCON) 2027, badala yake kuendelea kujifua.

Mbeya City ilianza vyema msimu kwa takribani mechi nne, kabla ya mambo kuwatibukia na kujikuta wakicheza michezo sita mfululizo bila ushindi na baadaye juzi kufufuka kuilaza Singida Black Stars bao 1-0.

MBE 01

Matokeo hayo yalionekana kurejesha furaha ndani na nje ya uwanja, kutokana na kujinasua nafasi za chini na kupanda nafasi ya 11 kwa pointi 13 baada ya michezo 11 iliyocheza kwenye ligi hiyo.

Timu hiyo inatarajia kurudi uwanjani Novemba 20 itakapowafuata Namungo mkoani Lindi kabla ya kurejea nyumbani uwanja wa Sokoine kuwakaribisha bingwa mtetezi, Yanga Novemba 27.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga amesema tatizo kubwa lililowapitisha kwenye ugumu ni kukosa kujiamini na presha kubwa, akieleza kuwa ushindi dhidi ya Singida BS umerejesha nguvu mpya.

Amesema kutokana na matokeo hayo, anahitaji kuona kila mchezaji akiendeleza ubora huo haswa kutoruhusu bao kama ilivyokuwa michezo iliyopita akisisitiza kuwa anataka kasi ya mabao.

MBE 02

“Tulicheza kwa hofu na wasiwasi ikatugharimu kupoteza mechi nyingi, kwa sasa tumerejea vizuri tukishinda bila kuruhusu bao, nataka mwendelezo huu tukisaka mabao ya kufunga” amesema Mayanga.

Kocha huyo ameongeza kuwa ligi ni ngumu japokuwa lazima wakabiliane na mpinzani yeyote bila kujali wanacheza ugenini au nyumbani na mkakati wao ni kila mechi vita ya pointi tatu.