Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shikangwa awasha moto Misri

SHIKANGWA Pict

Muktasari:

  • Shikangwa alitia kambani mabao hayo katika dakika ya 15, akiipatia FC Masar bao la kuongoza ambalo lilidumu hadi mapumziko, dakika ya 74 aliiandikia timu hiyo bao la pili baada ya kupokea pasi ya Aissatou Ba.

MSHAMBULIAJI wa FC Masar ya Misri, Jentrix Shikangwa juzi Novemba 04, 2026 alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 walioupata timu hiyo dhidi ya FUS Rabat ya Morocco katika mchezo wa pili wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.

Shikangwa alitia kambani mabao hayo katika dakika ya 15, akiipatia FC Masar bao la kuongoza ambalo lilidumu hadi mapumziko, dakika ya 74 aliiandikia timu hiyo bao la pili baada ya kupokea pasi ya Aissatou Ba.

Katika mashindano hayo makubwa ya kumtafuta bingwa wa Afrika Simba Queens ambayo ilishiriki michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ilimaliza hatua ya makundi ikikusanya pointi tatu wakati ambao Shikangwa alikuwa tayari amehamia Masar.

Hata hivyo, mabao hayo mawili aliyofunga ni muendelezo wa kiwango cha Shikangwa ambaye amekuwa na rekodi nzuri ya ufungaji tangu alipokuwa akiitumikia Simba Queens.

SHIKA 01

Shikangwa alijiunga na Simba Queens Septemba 2022 akitokea Vihiga Queens ya Kenya na katika misimu minne aliyocheza akiwa na kikosi hicho alifanikiwa kufunga mabao 69 katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.

Takwimu hizo zinamuweka miongoni mwa washambuliaji wa kigeni walioacha alama kubwa katika historia ya soka la wanawake nchini, huku uwezo wake wa kufunga katika michezo mikubwa ukiwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Simba Queens.

Akiwa Msimbazi, Shikangwa alifanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya Wanawake katika misimu ya 2023/24 na 2025/26, lakini pia msimu wa 2023 aliibuka mfungaji bora akiweka kambani mabao 17.

Mbali na mataji hayo ya ligi, mshambuliaji huyo pia alisaidia Simba Queens kutwaa ubingwa wa CECAFA na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake msimu wa 2023/24.

SHIKA 02

KUFUATA NYAYO ZA UBAMBA?

Kiwango anachoonyesha mshambuliaji huyo huenda akafuata nyayo za Mtanzania Hasnath Ubamba ambaye aliwahi kufanya vizuri katika kikosi hicho cha Misri.

Ubamba, ambaye alikaa FC Masar kwa misimu miwili, alicheza jumla ya mechi 50, akifunga mabao 30 na kutoa asisti 19, takwimu zilizomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi hicho.

Katika kipindi chake, Ubamba alisaidia FC Masar kutwaa mataji mawili mfululizo ya Ligi Kuu ya Misri na kufanya vizuri katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.

Uwepo wa Shikangwa na rekodi alizoanza kuziandika FC Masar sasa unaendeleza simulizi ya wachezaji waliotoka Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania na kwenda kuonyesha uwezo wao katika soka la Misri.