Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi kumi Dodoma Jiji inakimbiza kimyakimya

DODOMA Pict

Muktasari:

  • Dodoma imepiga hatua kubwa ikilinganishwa na ilivyoanza msimu uliopita, jambo linaloonekana kupitia idadi ya ushindi, mabao na pointi ilizokusanya katika michezo 10 ya mwanzo.

WAKATI Simba ikiendeleza moto kwenye Ligi Kuu Bara, Dodoma Jiji msimu huu nayo ni kama inakimbiza mwizi kimya kimya kutokana na rekodi iliyoiweka kwenye mechi 10 za mwanzo.

Dodoma imepiga hatua kubwa ikilinganishwa na ilivyoanza msimu uliopita, jambo linaloonekana kupitia idadi ya ushindi, mabao na pointi ilizokusanya katika michezo 10 ya mwanzo.

Msimu uliopita, timu hiyo ilianza kwa kusuasua, kwani katika michezo 10 ya kwanza iliambulia ushindi miwili, sare nne na vipigo vinne, hali iliyoifanya ikusanye pointi 10 kati ya 30 zilizokuwa kwenye hesabu.

Tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, msimu huu Dodoma Jiji imekusanya pointi 16 katika michezo 10, ikishinda minne, kutoka sare nne na kupoteza miwili, ikiwa imeongeza pointi sita zaidi ya ilizopata msimu uliopita.

Rekodi ya kukusanya pointi hizo inafanana na msimu wa 2021/22 pia ilikuwa na pointi 16, lakini ilifunga mabao tisa na kuruhusu sita.

DOM 01

Mwanzo mbaya zaidi ulikuwa msimu wa 2022/23, ilipokusanya pointi sita pekee, ikiwa na ushindi mmoja, sare tatu na vipigo sita.

Katika eneo la ushambuliaji, Dodoma Jiji pia imekuwa na ufanisi. Msimu uliopita ilifunga mabao sita katika michezo hiyo, lakini msimu huu imefunga mabao nane, ikiwa ni ongezeko la mabao mawili.

Mabao hayo yamechangia kuifanya timu hiyo ipate matokeo mazuri zaidi, huku ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold ukiwa miongoni mwa matokeo yaliyoipa ushindi mnono zaidi.

Eneo lingine ambalo Dodoma Jiji imeonyesha mabadiliko ni safu ya ulinzi. Katika michezo 10 ya mwanzo msimu uliopita, iliruhusu mabao 10, lakini msimu huu imeruhusu mabao matano pekee, ikiwa imepunguza nusu ya mabao ya kufungwa.

DOM 02

Hiyo ina maana kuwa kwa wastani, msimu uliopita Dodoma Jiji ilikuwa ikiruhusu bao moja kwa kila mechi, wakati msimu huu wastani wake umeshuka, takwimu zinazoonyesha tofauti katika uimara wa safu yake ya ulinzi.

Kwa upande wa matokeo, msimu huu Dodoma Jiji imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya TRA United, Mashujaa, Namungo na Geita Gold, huku ikipata sare dhidi ya Pamba Jiji, Singida Black Stars, JKT Tanzania na Coastal Union. Vipigo vyake viwili dhidi ya Mbeya City na Polisi Tanzania.

Msimu uliopita timu hiyo ilimaliza ikikusanya pointi 35 wastani wa nusu ya ilizokusanya msimu huu kwenye mechi 10 tu za mwanzo.

Dodoma Jiji imeonyesha maendeleo makubwa katika maeneo matatu muhimu, ukusanyaji wa pointi, ufungaji mabao na uimara wa ulinzi. Ikiwa itaendeleza mwenendo huo, itakuwa na nafasi ya kujiweka katika mazingira bora zaidi ya kumaliza msimu huu kwenye nafasi nzuri kuliko ilivyokuwa msimu uliopita.