Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Yanga wapewa ishu za kocha mpya

SAA chache tu baada ya Mwanaspoti kufichua kuwa mabosi wa Yanga wapo mbioni kumleta Kocha Mfaransa Sebastien Migne anayetarajiwa kutua nchini ndani ya wiki, mastaa wa timu hiyo wamepewa mchongo mzima juu ya kocha huyo ikielezwa jamaa huyo ni fundi.

Siri juu ya kocha imefichuliwa na mmoja ya mastaa waliofanya naye kazi aliyepo Jangwani kwa sasa, kipa Faruk Shikhalo aliyedai ameshtuka kwa furaha kusikia jamaa anakuja na kusisitiza Migne ni jembe.

Shikhalo aliwafichulia wenzake kwa kuliambia Mwanaspoti kama jamaa anakuja Yanga, basi wajipange kwelikweli kocha huyo ana mambo matatu ambayo huwa hana mchezo nayo.

Kipa huyo kutoka Kenya alisema Migne atakuja kumaliza utata wa matokeo, ila akaongeza akisema jamaa ni bonge la kocha.

Shikhalo alisema ingawa hajapata uhakika kama Migne anakuja ila endapo atatua kikosini anatarajia awe kocha muafaka kwa nyakati hizi katika timu yao na kwamba mabosi wake watakuwa wamepiga bao.

“Kwa hali tulionao kama Migne atatua hapa nadhani ni mtu muafaka kabisa kwetu, unajua huyu ni kocha mwenye uwezo wa kubadilisha mambo kwa haraka na tukakaa sawa,” alisema Shikhalo aliyefundishwa na Migne akiwa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars na kuwapeleka Afcon 2019.

Mbali na Shikhalo Wakenya wengine waliopo nchini walionoelewa na Migne ni beki Simba Joash Onyango na kiungo wake Francis Kahata, wote wakiiitwa wakitokea Gor Mahia na Shikhalo Bandari FC.

“Akija Migne itapendeza akiendelea na kocha Mwambusi (Juma), unajua Mwambusi amekaa nasi kwa muda mrefu na atamsaidia sana kuweza kuanza vyema. Kwa jinsi ninavyowajua kuna hatua kubwa itakuwa imepigwa,” alisema Shikhalo.

Aliongeza, kitu cha pili ambacho Migne atakibadilisha ni nidhamu akisema Mfaransa huyo hataki utani katika nidhamu hasa nje ya uwanja, pia kama hujali muda utaingia matatani mbele yake.

“Huyu ni kocha, akisema saa sita iwe saa sita ukiwahi kabla ya hapo ni faida kwako, lakini ukichelewa hajui kuonya, yeye ni adhabu tu, hataki mambo ya nidhamu mbovu iwe ndani ya timu au nje ya uwanja hayo hayavumiliki kwake,” alisisiriza Shikhalo.

Akizungumzia soka lake Shikhalo alisema kocha huyo wa zamani wa DR Congo, Togo na Guinea ya Ikweta ni muumini wa soka la kushambulia la pasi nyingi, kitu ambacho wapinzani wao wasipokuwa makini wataipata freshi kwani moto wa Yanga utakuwa marudufu safari hii.

“Tulikuwa na kocha Kaze, naye alipenda soka la kushambulia, lakini Migne naweza kusema ni zaidi yake na hataki mambo ya kucheza bila faida, anapenda pasi ziwe nyingi ila mpira uende mbele kutafuta matokeo, kitu ambacho naamini kitatubeba tukiwa chini yake,” alisema Shikhalo na kuongeza;

“Ukiwa beki hataki kufanyike makosa ya kuchezea mpira ukiwa mtu wa makosa huwezi kucheza katika timu yake,anapenda uwe makini muda wote.”

Yanga ipo mbioni kuleta kocha mpya baada ya kuachana na Kaze aliyeiongoza timu hiyo katika mechi 18 na kupatas ushindi michezo 10, huku saba ikiambulia sare na kupoteza moja dhidi ya Coastal Union, ikikomaa kileleni na jumla ya ponti 50 kwa kucheza mechi 23.