Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masoud na matumaini mapya Songea United

MASOUD Pict

Muktasari:

  • Baada ya Stand kuitoa Geita Gold, ikacheza 'Play-Off' nyingine na Fountain Gate iliyotolewa pia hatua hiyo na maafande wa Tanzania Prisons kwa jumla ya mabao 4-2, ambapo kikosi hicho kilikwama kupanda baada ya kufungwa jumla ya mabao 5-1.

KOCHA Mkuu wa Songea United ya Songea, mkoani Ruvuma, Juma Masoud amesema anahitaji muda zaidi kwa ajili ya kutengeneza timu ya ushindani, baada ya kikosi hicho kuchelewa kuanza mapema maandalizi ya msimu wa 2026-2027, yaani (Pre Season).

Akizungumza na Mwanaspoti, Masoud aliyewahi kuifundisha FGA Talents kwa sasa Fountain Gate, amesema timu hiyo ilichelewa kuanza maandalizi ya msimu kutokana na baadhi ya wachezaji kuchelewa kuripoti kambini, ingawa kila kitu kinaenda vizuri.

"Tuna maingizo mapya ya wachezaji kwa ajili ya msimu wa 2026-2027 na taratibu tumeanza kutengeneza muunganiko mzuri wa kiuchezaji, Ligi ya Championship ni ngumu na ili kuendana nayo ni lazima tujipange mapema iwezekanavyo," amesema Masoud.

Masoud aliyejiunga na Songea United Januari 2026, akichukua nafasi ya Meja Mstaafu, Abdul Mingange aliyeanza nayo msimu wa 2025-2026, kabla ya mechi ya jana dhidi ya Rhino Rangers.

Msimu wa 2024-2025, Masoud akiifundisha Stand United, aliiongoza kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi ya Championship na pointi 61, jambo lililoiwezesha kucheza mechi za 'Play-Off' za kusaka tiketi ya kupanda Ligi Kuu Bara, ingawa, alikwama.

Stand United iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu msimu wa 2018-2019, ilianza kucheza 'Play-Off' ya kwanza kwa kishindo kwa kuiondosha Geita Gold kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya kikosi hicho cha mjini Geita kumaliza nafasi ya nne na pointi 56.

Baada ya Stand kuitoa Geita Gold, ikacheza 'Play-Off' nyingine na Fountain Gate iliyotolewa pia hatua hiyo na maafande wa Tanzania Prisons kwa jumla ya mabao 4-2, ambapo kikosi hicho kilikwama kupanda baada ya kufungwa jumla ya mabao 5-1.