Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Ethiopia aondoka na hili CECAFA U-20

ETHIOPIA Pict

Muktasari:

  • Ethiopia ilianza mashindano hayo kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Rwanda, kabla ya kukutana na Tanzania katika mchezo wa pili wa Kundi A uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

KOCHA wa timu ya Taifa ya U-20 ya Ethiopia, Benjamin Ziemer amesema vijana wake walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga dhidi ya Tanzania, lakini walishindwa kuzitumia vizuri hali iliyowagharimu katika mchezo huo wa kufuzu AFCON U-20.

Ethiopia ilianza mashindano hayo kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Rwanda, kabla ya kukutana na Tanzania katika mchezo wa pili wa Kundi A uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo dhidi ya Tanzania, Ethiopia ilionekana kuwa na baadhi ya nafasi za kufunga, lakini ilishindwa kuzigeuza kuwa mabao, huku Tanzania ikitumia vyema nafasi zake na kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao mawili.

Ziemer amesema mabao hayo mawili ya kipindi cha kwanza yaliwaathiri kisaikolojia na kuwafanya washindwe kurejea katika mchezo baada ya mapumziko, jambo lililoifanya Tanzania itawale na kuongeza mabao mengine.

“Tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini hatukuzitumia vizuri. Tatizo lilikuwa kwenye umaliziaji wakati huo huo, tuliruhusu mabao mawili kipindi cha kwanza ambayo yalituchanganya na tukashindwa kurudi kwenye mchezo,” amesema Ziemer.

Kocha huyo ameongeza licha ya kuondolewa kwenye mashindano hayo lakini wamepata uzoefu na kujua namna gani ya kucheza na timu zenye ushindani na zilizofiti kama Tanzania na Uganda.

Kipigo hicho cha mabao 4-0 kimeifanya Ethiopia kuondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kupata pointi moja katika mechi mbili, huku Tanzania ikifuzu nusu fainali na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu AFCON U-20.