Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adeyum Saleh ajipanga upya Mbuni FC

ADEYOUM Pict

Muktasari:

  • Licha ya kucheza nafasi ya beki wa kushoto, ila Adeyum alishika nafasi ya pili kwa wachezaji wa Bigman FC waliofunga mabao mengi kwa msimu wa 2025-2026, baada ya kufunga matano, nyuma ya Mnigeria Collins Kelvin Nwobodo aliyefunga sita.

BEKI mpya wa kushoto wa Mbuni FC ya jijini, Arusha, Adeyum Saleh amesema amefikia uamuzi wa kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2026-2027, kwa lengo la kutafuta changamoto nyingine, baada ya kuachana na Bigman FC ya jijini, Tanga.

Akizungumza na Mwanaspoti, nyota huyo aliyewika na timu mbalimbali Yanga, Coastal Union, Stand United, Kagera Sugar na Dodoma Jiji, amesema licha ya ugeni wake katika kikosi hicho, ila anaamini uzoefu alionao utasaidia kutimiza malengo.

"Hatujaanza vizuri msimu huu, lakini bado tuna nafasi ya kufanya kitu kizuri mbeleni, ligi imeanza na ugumu kutokana na ushindani uliopo kwa kila timu na malengo iliyoweka, nitapambana kuongeza uzoefu na wachezaji wenzangu," amesema Adeyum.

Aidha, Adeyum amesema licha ya kucheza beki wa kushoto ila malengo yake msimu wa 2026-2027, ni kufunga zaidi mabao kila atakapopata nafasi ya kufanya hivyo, kama ilivyokuwa msimu wa 2025-2026, wakati akikichezea kikosi hicho cha Bigman FC.

Licha ya kucheza nafasi ya beki wa kushoto, ila Adeyum alishika nafasi ya pili kwa wachezaji wa Bigman FC waliofunga mabao mengi kwa msimu wa 2025-2026, baada ya kufunga matano, nyuma ya Mnigeria Collins Kelvin Nwobodo aliyefunga sita.