Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa iko tayari kuivaa Fountain Gate

MASHUJAA Pict

Muktasari:

  • Mashujaa ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, itaanza msimu dhidi ya Fountain ambayo ilimaliza nafasi ya tano.

Kocha wa Mashujaa Queens, Rajab Ally, amesema maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya Fountain Gate Princess yako vizuri, huku akieleza kuwa wachezaji wote wapo salama na tayari kwa mtihani huo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Rajab amesema kikosi chake kimekamilisha maandalizi kinaelekeza nguvu zake kwenye mchezo huo mgumu dhidi ya Fountain.

“Maandalizi ni mazuri, tunashukuru Mungu vijana wote wapo salama na tupo tayari kwa mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Fountain Gate Princess,”  amesema kocha huyo.

Rajab alifafanua kuwa kikosi chake kipo safarini kuelekea Dodoma, ambako kitakwenda kuwania matokeo mazuri katika mchezo huo wa ufunguzi utakaopigwa Jumatano Oktoba 28 Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kocha huyo pia alithibitisha kuwa msimu huu Mashujaa itautumia Uwanja wa NDC, uliopo Kunduchi kama uwanja wake wa nyumbani.

Mashujaa ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, itaanza msimu dhidi ya Fountain ambayo ilimaliza nafasi ya tano.