Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanasoka wa kike wapewa somo la mimba, soka

MIMBA Pict

INAELEZWA kwamba ili mimba isiwe kikwazo kwa wanasoka wa kike kutimiza ndoto zao, viongozi wa klabu wanatakiwa kutoa elimu ya maisha kwa wachezaji itakayowasaidia kufanya uamuzi sahihi kuhusu kuanzisha familia.

Mratibu wa Yanga Princess, Kibwana Matokeo anasema: “Huu ni mjadala mpana. Jambo ninaloona linahitajika ni elimu kwa viongozi wa klabu. Ninachomaanisha ni kwamba mchezaji akipata mimba hadi kujifungua, inamchukua takribani miaka miwili. Ili aweze kurejea kwa haraka, inatakiwa kusaidiwa. Wakati huo huo, timu nayo inatakiwa inufaike na mchezaji. Hata hivyo, elimu ikieleweka, itapatikana hamasa katika jambo hilo.”

Kocha wa Mashujaa, Amani Josiah, anashauri kuwa katika timu za wanawake kuwe na dawati maalumu linalotoa elimu ya maisha ili wachezaji wakielewa kwa kina maana ya familia, itakuwa rahisi kwao kujisimamia.

MIMB 08

“Katika mikataba yao, ni muhimu kuweka kipengele cha ulinzi pindi wanapopata mimba. Lakini kwanza waelewe na wawe na utayari wa kuwa na familia. Nje ya hapo, itakuwa vigumu kwa wengi wao kuzaa,”  anasema.

Mratibu wa Simba Queens, Seleman Makanya, anasema: “Ikitokea mchezaji akapata mimba akiwa na mkataba, hatuwezi kuuvunja, kwani tunaheshimu suala la wao kuanzisha familia zao. Lakini wengi wao, naona, ni waoga katika hilo.

Hivyo, jambo la msingi kwa wachezaji wenyewe ni kujua kwamba soka ni la muda mfupi, lakini familia ni sehemu ya maisha yao ya muda mrefu. Kwa hiyo, elimu ya mara kwa mara inahitajika kwao.”

Beki wa Mashujaa Queens, Mariam Yusuph Juma, mwenye umri wa miaka 33, ameolewa na amefanikiwa kupata watoto watatu akieleza njia alizotumia ambazo zimemsaidia kuendelea na majukumu yake hadi sasa, akiamini kuwa zitawasaidia na wengine.

MIMB 05

“Mwanangu wa kwanza nilimzaa mwaka 2012 nikiwa katika kituo cha Marsh Queens. Wakati mwanangu bado mdogo nilipata timu ya Kinondoni iliyokuwa inacheza Taifa Cup. Nilipokuwa naingia mkataba nao, niliwaambia lazima wazingatie suala la mtoto wangu. Hivyo, nikawa nakaa naye kambini, na walinitafutia mtu wa kumhudumia nikiwa mazoezini au kwenye mechi,”  anasema na kuongeza:

“Mwaka 2015 nilisajiliwa na Mburahati Queens, kipindi hicho nikiwa mchezaji wa daraja la juu. Tulikuwa tunapewa Sh. 100,000 na viatu, lakini hakukuwa na mshahara. Nilipopata mimba ya mtoto wangu wa pili, niliendelea kufanya mazoezi na timu hadi ilipofika miezi saba. Kisha nikaomba nirudi nyumbani ili nikasubiri muda wa kujifungua. Niliwaweka wazi viongozi kuwa nimeolewa, hivyo hakuna namna nitakavyoweza kukwepa kukutana kimwili na mume wangu.

“Baada ya kujifungua, mwanangu alipofikisha umri wa mwaka mmoja, nilisajiliwa na Kigoma Sisters kwa mkataba wa misimu miwili, 2016/17 na 2017/18. Sharti nililowaambia viongozi ni kwamba nitasaini mkataba wa watu watatu. Mwanangu niliyemuacha nyumbani, kila mwezi itumwe Sh200,000 kwa matumizi yake, na mwanangu ambaye nilikuwa naye kambini atafutiwe dada wa kazi, huku akizingatiwa katika lishe na matibabu. Walifanya hivyo, nikaendelea na majukumu yangu.”

MIMB 07

Anasema baada ya kumaliza mkataba na timu hiyo, alirejea kuichezea Marsh Queens, lakini mwaka 2020 alipata tena mimba.

“Nilipata mimba ya mtoto wangu wa tatu, ambayo ilinifanya niwe naumwaumwa. Ilipofika miezi mitatu, ilibidi niwaambie viongozi ili nikajisikilizie nyumbani,”€  anasema na kuongeza:

“Baada ya kujifungua, mwanangu alipofikisha miezi mitatu, viongozi wa timu ya Tiger Queens walinifuata ili wanisajili. Nikawaambia ukweli kwamba nina mtoto mwenye miezi mitatu. Kama watanichukua, nitaingia mkataba wa mimi na mwanangu.

“Walikubali, nikaenda na mwanangu kambini na nikatafutiwa dada wa kumtunza. Nilifanya vizuri hadi nikaitwa Twiga Stars mwaka 2021, timu iliyochukua taji la Cecafa Afrika Kusini. Hivyo, kilichonibeba ni kuweka vipengele vya kunilinda katika mikataba yangu.”

Kocha wa Simba Queens, Hassan Mgosi, anasema: “Jambo la msingi ni wachezaji kujitambua. Soka haliwezi kuwa kikwazo kwao kuanzisha familia zao, kama ilivyo ajira kwa wanasoka wa kiume. Mfano ni mimi mwenyewe; nimecheza soka na nina familia. Binafsi, nimekuwa nikiwapa elimu ya mara kwa mara kwamba soka haliwezi kubadilisha uhalisia wao.”