Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga ngoma ngumu Arusha

ARUSHA Pict (1)

Muktasari:

  • Suluhu ya Yanga imeibua presha kubwa kwa kocha mkuu Manqoba Mngqithi baada ya mashabiki wa timu hiyo kuonyesha wazi hawana imani naye katika mitandao ya kijamii, na wengine uwanjani hapo suala linaloongeza uwezekano wa kutoendelea tena kikosini.

MTAAMBIA nini watu! Ndivyo unavyoweza kusema kwa sasa baada ya Yanga kushindwa kutamba katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya TRA United iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kumalizika kwa suluhu.

Suluhu ya Yanga imeibua presha kubwa kwa kocha mkuu Manqoba Mngqithi baada ya mashabiki wa timu hiyo kuonyesha wazi hawana imani naye katika mitandao ya kijamii, na wengine uwanjani hapo suala linaloongeza uwezekano wa kutoendelea tena kikosini.

Katika ukurasa wa kijamii wa Yanga wa Instagram, mashabiki wa timu hiyo walionyesha kutofurahia kiwango cha kikosi hicho kwa sasa, jambo lililoanza tangu ilipochapwa na watani zao wa jadi Simba kwenye mechi ya ‘Kariakoo Derby’ ya Oktoba 10, 2026.

Katika mechi hiyo, Yanga ilishindwa kutumia vyema nafasi mbalimbali ilizotengeneza huku wachezaji wa kikosi hicho wakishindwa kuonyesha kiwango cha kuvutia, huku wakienda hadi dakika ya 60 bila kupiga shuti lolote.

SHE 01

Mapema dakika ya 32, Yanga ilinusurika kupata bao la utangulizi lililofungwa na mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Seleman Mwalimu ‘Gomez’, ingawa, lilishindwa kusimama baada ya msaada wa Teknolojia ya Football Video Support maarufu (FVS). Bao hilo lilifungwa kwa ustadi wa hali ya juu na Mwalimu akiunganisha mpira huo kwa kichwa akipokea pasi ya Mudathir Yahya, ingawa kwa msaada wa FVS, lilikataliwa, baada ya winga wa TRA United, Franck Steve Belobo kuchezewa madhambi.

Sare hiyo ni ya kwanza kwa Yanga katika Ligi Kuu Bara tangu msimu huu umeanza, baada ya kushinda sita za mwanzoni na kuchapwa moja kati ya nane iliyocheza na kuirahisishia watani zao Simba inayoongoza katika msimamo na pointi zake 24.

Matokeo ya leo yanaifanya Yanga kufikisha pointi 19, baada ya kucheza mechi nane sawa na za Simba inayoongoza ikiwa na 24, kufuatia kushinda zote, jambo linalowafanya mabingwa hao watetezi kwa sasa kupitwa na gepu la jumla ya pointi tano.

SHE 02

Hata hivyo, TRA United ilishindwa kutumia nafasi za kuifunga Yanga baada ya kiungo nyota wa timu hiyo, Mudathir Yahya kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90, kufuatia kumzuia Abdulhamid Juma aliyekuwa anaenda kufunga akiwa mchezaji wa mwisho.

Sare hiyo ni ya kwanza kwa Kocha Mkuu wa TRA United, Hemed Suleiman ‘Morocco’, tangu ajiunge na kikosi hicho, Septemba 10, 2026, akirithi nafasi ya Mrundi Etienne Ndayiragije aliyeondoka kwa makubaliano ya pande mbili, Septemba 7, 2026.

Kocha huyo alianza kwa ushindi na kikosi hicho wa mabao 3-1, dhidi ya Pamba Jiji, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini, Mwanza, Septemba 13, 2026, kisha akachapwa na Namungo FC 1-0, Oktoba 8, 2026, kwenye Uwanja wa Majaliwa, mkoani Lindi.

Kwa ujumla TRA imecheza mechi nane Ligi Kuu Bara, ambapo kati ya hizo imeshinda moja, sare nne na kupoteza tatu, ikiwa nafasi ya 12 na pointi saba, huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao sita na kuruhusu saba.

SHE 03

Haya siyo matokeo mazuri kwa Yanga ambayo imeshatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo.


MASHABIKI MAONI MSETO

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Yanga, baadhi ya mashabiki wa timu hiyo walionekana kutoridhika na jinsi ilivyokuwa ikicheza huku wakitaka taarifa ya umma itoke haraka kwa kuwa wanaona kikosi chao hakina kasi, mashambulizi hafifu, lakini timu haivutii ambapo baadhi ya maoni yao yalikuwa hivi:

Agent-kai4: “Mfumo mbovu.. double striker mfumo wa zama za mawe”

Wakili-1msomi: “Kocha atuache tu”

Msikola9: “Atuna kocha”

Alkha-menei: “Huyu kocha bila kumtimua uyu sawaa”

Elijah Moshi: “Fitness kocha na kocha mkuu watupishe”

Afyatop: “No shot on target”

Mussafries: “Mechi tano za kwanza timu ilikuwa inatengeneza nafasi nyingi,na kupata magoli machache sasa hivi timu kupata shoot on target changamoto.”

SHE 04

Mabulanta: “Kwamba mankoba ni kocha wa boli sio aina noma..”

Frankmzito: “Sema kwa kocha uyu wanangu bila shaka tutakua tunashinda kwa mbinde na pira bumunda.”