Mashabiki Mtoko wa Kibingwa walivyoisubiri dabi kivingine
Hakuna mbambambaa! ndivyo mashabiki 100 wa Simba na Yanga walioibuka mabingwa wa promosheni ya Betika Mtoko wa Kibingwa walivyotamka jana usiku wakati wakisherehekea bata la msimu lililokuwa mahususi kwa ajili ya kuisubiri mechi ya dabi ya watani wa jadi Simba na Yanga leo.
Kabla ya mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam jioni hii ya Aprili 16, Mabingwa hao kutoka mikoa mbalimbali nchini walianza kwa kusherehekea bata la msimu huku wakitambiana kila upande ukijinasibu kuondoka na pointi tatu kwenye mechi hiyo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabingwa kutoka mikoani, waliwasili Dar es Salaam jana asubuhi na juzi usiku kwa ndege na kungana na wale wa Dar es Salaam jioni katika pati ya bata la msimu iliyofanyika Kidimbwi ikinogeshwa na msanii maarufu, Christian Bella,
Dj d Ommy, Mussa Husein, Ibra Kasuga na Abby Chams.
Kampuni ya Betika Tanzania imewagharamia mabingwa hao 100 ambao walishinda promosheni ya Mtoko wa Kibingwa kuishuhudia dabi hiyo kwa hadhi ya VIP leo, huku jana wakishiriki hafla hiyo iliyokwenda sanjari na burudani mbalimbali.
Sherehe hiyo ilifanyika kwa saa 4 kuanzia saa 2 usiku hadi saa 6 likiwa na burudani ya muziki, mashabiki wa pande zote mbili kutambiana na wachambuzi kuichambua dabi hiyo na burudani nyingine zilizonogesha sherehe hiyo.
Ofisa habari wa Betika Tanzania, Juvelinaus Rugambwa amesema leo Jumapili mabingwa hao watakwenda kwa Mkapa wakiongozwa na king'ora kuishuhudia dabi hiyo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara wakiwa VIP.
Hii ni mara ya tano kwa Betika kuleta mabingwa wa promosheni ya Mtoko wa Kibingwa kushuhudia dabi hiyo laivu huku kila msimu idadi ikiongezeka na safari hii ni mara mbili ya ile ya awali.
"Tukisema Mtoko wa Kibingwa, maana yake ni hii, imekuwa ni bandika bandua kwa washindi wetu ambao walipokelewa kibingwa Ijumaa na Jumamosi na kufikia kwenye hoteli ya nyota tano.
"Jumamosi kama ratiba ilivyokuwa imepangwa, walishiriki kwenye bata la msimu na kulala kwenye hoteli ya nyota tano na leo Jumapili wataishuhudia dabi laivu kwa Mkapa," amesema