Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mara paap! Zlatan katua Everton

LIVERPOOL ENGLAND. ZLATAN Ibrahimovic yupo sokoni, kumpata ni pesa yako tu. Na sasa kinachoelezwa ni kwamba staa huyo huenda akawashtua wengi baada ya kudaiwa yupo njiani kwenda Everton kuungana na Kocha Carlo Ancelotti ikiwa ni bonge la dili la kijanja linalotajwa kwenda kutokea Goodison Park.

Supastaa huyo fowadi kwa sasa hana timu baada ya mkataba wake kumalizika huko LA Galaxy tangu mwishoni mwa Novemba.

Lakini, sasa anaweza kuibukia tena kwenye Ligi Kuu England kama atakubaliana na ombi la Ancelotti, anayemtaka wakapige kazi kwenye kikosi cha Everton. Ibra aliwahi kuitumikia Manchester United kwenye ligi hiyo.

Kocha Ancelotti anadaiwa amebakiza mambo machache tu kabla ya kukubali dili la kwenda kuinoa Everton kwa dili la mshahara wa Pauni 11.5 milioni kwa mwaka.

Mtaliano huyo anataka usajili wake wa kwanza uwe mshambuliaji veterani ili kwenda kuongoza safu ya ushambuliaji kuirudisha timu kwenye nafasi za juu katika msimamo wa ligi baada ya mambo kuwa hovyo sana.

Ancelotti anafahamu ugumu wa Ligi Kuu England na huduma yake imekuwa ikiwindwa na wengi hata kabla ya kufunguliwa mlango wa kutokea huko Napoli.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari Mtaliano, Tancredi Palmeri, AC Milan inamtaka pia straika Ibrahimovic kurudi kupiga kazi huko San Siro. Lakini, shida ni kama itaweza kushindana na mshahara wa Everton, ambayo inaonekana kuwa na mkwanja mrefu wa kuwabeba mastaa hao wawili (kocha na mchezaji).

Ibra, ambaye amefunga mabao 29 katika mechi 53 alizochezea Manchester United, hivi karibuni alionekana huko Beverley Hills, Marekani huko akidaiwa amekuwa kwenye mazungumzo ya kujiunga na Everton na kila kitu kinaonekana kwenda sawa.

Wiki iliyopita wakala wake Mino Raiola alisema: “Hatusemi kwamba itakuwa muhimu sana kurudi Italia. Timu gani kati ya tatu zinazomtaka atakwenda kujiunga? Hatujui, sisi ni watu huru.

“Kujiuzulu? Sitaki kusema chochote, lakini hilo halionekani kutokea. Ibra bado yupo vizuri kinoma.”

Kuwasili kwa Ibrahimovic kwenye kikosi cha Everton kutampa Ancelotti nguvu zaidi kwenye matakwa yake na kutaka kuwa na nguvu kwenye suala la mchezaji gani aje kusajili. Kwa sasa bosi anayesimamia usajili wote Everton ni Marcel Brands, ambapo ndani ya misimu miwili iliyopita ametumia Pauni 200 milioni na matunda hayakuonekana. Mshahara huo wa Ancelotti, kwa mwezi atakuwa analipwa Pauni 958,333, wiki Pauni 221,153, kwa siku Pauni 31,593 kwa saa Pauni 1,316 na kwa dakika ni Pauni 21.