Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamadou Sakho kuendeleza soka Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza hatua ya chezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL), Mamadou Sakho ya kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa Zanzibar.

Rais Mwinyi alitoa pongezi hizo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo nyota huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Katika mazungumzo hayo, Rais Mwinyi alieleza kwamba huo ni mwanzo mzuri katika kuinua na kuendeleza vipaji vya michezo vya vijana wa Zanzibar.

Mamadou ambaye ni mara ya pili kuitembelea Zanzibar, aliambiwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana nae katika kuanzisha kituo hicho cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alimueleza mchezaji huyo kuwa ujio wake una  umuhimu mkubwa katika kuutangaza utalii wa Zanzibar pamoja na vivuto vilivyopo.

Kwa upande wake Mamadou Sakho ambaye amefuatana na Mkewe Majda Sakho alisema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo ya kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo Zanzibar kwa kutambua kwamba ana deni  na wajibu mkubwa wa kuleta maendeleo Afrika akijuwa kwamba yeye ni Mwafrika licha ya kwua amezaliwa Ufaransa na anabeba uraia wa Taifa hilo.

Aliongeza kuwa ameichagua Zanzibar kuwa ni eneo maalum kwa kuanzisha kituo hicho kitakachoendeleza soka hapa nchini.