Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makata abanwa na mawili Polisi

MAKATA Pict

Muktasari:

  • Polisi Tanzania imecheza mechi 11, ikishinda nne, sare tatu na kupoteza nne, huku ikiwa imekusanya pointi 15, ikifunga mabao 13 na kuruhusu 12. Kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Mbwana Makata amebaini maeneo mawili yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa nguvu kubwa katika kikosi chake, licha ya timu hiyo kurejea kwenye ushindi katika mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu Bara.

Polisi Tanzania imecheza mechi 11, ikishinda nne, sare tatu na kupoteza nne, huku ikiwa imekusanya pointi 15, ikifunga mabao 13 na kuruhusu 12. Kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

Ushindi wa Geita Gold ulikuwa muhimu kwa Polisi kurejea kwenye matokeo mazuri baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Namungo, Oktoba 29, huku kabla ya hapo ikitoka sare ya bao 1-1 na Pamba Jiji.

Polisi imerejea mazoezini baada ya kupewa mapumziko ya siku tatu, huku ikitaka kutumia muda wa mapumziko ya kalenda ya FIFA kama muda wa kuendelea kujinoa.

POLI 01

Akizungumza na Mwanaspoti Makata amesema ameelekeza nguvu zake katika kuboresha umaliziaji wa nafasi za mabao pamoja na uimara wa safu ya ulinzi, akiamini kuwa maeneo hayo yana umuhimu mkubwa katika kuifanya timu yake kuwa imara zaidi kwenye michezo ijayo.

Makata amesema “Tunatengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini bado hatujawa na kasi nzuri ya kuzitumia. Hili ni eneo ambalo tunahitaji kulifanyia kazi kwa sababu kwenye mpira kutengeneza nafasi pekee hakutoshi, tunatakiwa pia kuzifunga,” amesema Makata.

Eneo la pili analolitazama kwa karibu ni safu ya ulinzi, ambayo amesema bado haijafikia kiwango anachokihitaji, hasa katika namna wachezaji wanavyocheza kwa utulivu wanapokuwa chini ya presha ya wapinzani.

Amesema ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya Geita Gold Novemba Mosi, bila kuruhusu bao, ni matokeo mazuri, lakini hauondoi umuhimu wa kuendelea kuboresha safu hiyo.

POLI 01

“Bado kuna mambo ya kurekebisha kwenye safu yetu ya ulinzi. Nataka kuona wachezaji wanakuwa watulivu zaidi wanapokuwa na mpira na wanapokabiliana na mashambulizi ya wapinzani. Hata kama mchezo uliopita hatukufungwa, bado tunahitaji kufanya vizuri zaidi,” amesema.

Mtihani mwingine kwa Makata na vijana wake baada ya mapumziko hayo ni dhidi ya Yanga Novemba 20, 2026, Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Huo utakuwa mchezo muhimu kwa Polisi kupima maboresho ya maeneo hayo mawili, hasa wanapokutana na wapinzani wenye uwezo mkubwa.