Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makambo apiga bao la kideo

Makambo apiga baa la kideo

Unguja. Mshambuliaji wa Yanga Haritier Makambo ameiongoza timu yake kwenda mapumziko ikiwa na bao moja alilolifunga kiufundi dakika 32 akipiga shuti la mbali lililomshinda kipa wa Taifa Jang'ombe Hussein Abel.

Makambo alifunga bao bora lililowainua mashabiki wake ikiwa dakika ya tatu aliikosesha timu yake bao akipiga shuti lililotoka nje ya goli akiwa na kipa.

Taifa Jang'ombe wameonekana kushambuliwa zaidi kipindi cha kwanza ambapo dakika ya 27 Yanga ililishambulia lango la wapinzani wao ingawa nao walifanikiwa kunusuru hatari hiyo langoni mwao.

Hata hivyo, Taifa Jang'ombe walijitahidi kupambana na wapinzani ambao hii ndio mechi yao ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi huku kiungo mpya Abubakar Salum 'Sure Boy' akilishika vyema dimba la kati.

Kwa upande wa kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery hakupata kashikashi nyingi kutoka kwa wapinzane wake kwani ngome yake ya ulinzi chini ya Bakari Mwamnyeto ilionekana kuwa imara zaidi.

Taifa Jang'ombe hii ni mechi yao ya pili baada ya ile ya awali kufunga na KMKM bao 2-1 ambapo Yanga itacheza mechi yao pili Ijumaa na KMKM