Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeraha yamtesa mshambuliaji ghali wa Singida United

Muktasari:

  • Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na uongozi wa Singida United baaada ya mahojiano na mwandishi waliweka bayana kwamba mchezaji huyo amerejea nchini Rwanda kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Dodoma. Mshambuliaji wa kimataifa wa Singida United, Danny Usengimana ameikosa mechi ya jana ya Singida United na Mbao FC jambo lililozua maswali kwa mashabiki wa timu hiyo.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na uongozi wa Singida United baaada ya mahojiano na mwandishi waliweka bayana kwamba mchezaji huyo amerejea nchini Rwanda kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

 Mchezo wa jana Jumapili Singida iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, huku uongozi wakisisitiza hawana tatizo na mchezaji huyo bali ni matatizo ya kiafya.