Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madaktari wamzuia Ronaldo kucheza, Messi bado mgonjwa

Muktasari:

  • KATIKA toleo lililopita, mwandishi Luca Caioli alielezea majanga ya kuumia yaliyomkuta Messi hali iliyoibua wasiwasi na uvumi ukihusisha aina ya vyakula alivyokuwa akila mchezaji huyo pamoja na aina ya nyama choma za Argentina na matatizo yake na mtaalama wake wa viungo. Endelea…

KATIKA toleo lililopita, mwandishi Luca Caioli alielezea majanga ya kuumia yaliyomkuta Messi hali iliyoibua wasiwasi na uvumi ukihusisha aina ya vyakula alivyokuwa akila mchezaji huyo pamoja na aina ya nyama choma za Argentina na matatizo yake na mtaalama wake wa viungo. Endelea…

Wako wengine waliohusisha kuumia huko na matatizo ya kisaikolojia, na wengine walihusisha kuumia huko na tofauti zilizoibuka kati yake na Juanjo Brau ambaye kwa muda mrefu ameendelea kuwa ndiye mtaalam wake wa viungo.

Wiki nane baadaye alirudi uwanjani akiwa katika kikosi kilichokuwa kinacheza mechi ya kwanza ya Kombe la Mfalme dhidi ya Getafe, alianzia benchi na kuingia katika dakika ya 61 wakati Barca tayari ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Katika dakika 30 aligusa mpira mara 36 na kutoa pasi nzuri 19 na kufumua mashuti manne yaliyokwenda vizuri langoni na kati ya hayo mawili yalizaa mabao. “Amerudi kulipa kisasi,” alisema Tata Martino, kocha mpya wa Barca kutoka Argentina.

Hata hivyo hadi katikati ya mwezi Februari kulikuwa na hofu baada ya kutapika katika mechi ya Kombe la Mfalme dhidi ya Real Sociedad Imewahi kumtokea mara chache hapo kabla na amekuwa akiendelea kucheza kama vile hakuna kilichomtokea, pamoja na hilo bado ni dhahiri kwamba kiafya hapo kuna tatizo, na mashabiki pamoja na vyombo vya habari vilikuwa na shauku ya kutaka kujua kulikoni hasa.

“Sijui hii ni nini, nimefanya vipimo ‘maelfu kwa maelfu’ kuna wakati inanitokea kabla ya mechi, natapika na kujiona kama mgonjwa lakini baadaye najiona niko vizuri tu.

Kutokana na kukosa taarifa rasmi mashabiki na wachambuzi wa soka wakawa wanakuja na tafsiri zao kuhusu tukio hilo. Wako waliokuwa wakisema kutapika huko kulitokana na homoni ambazo Messi alikuwa akitumia tangu akiwa kijana mdogo alipokuwa na tatizo la udumavu, ingawa mtaalamu aliyesimamia tiba yake utotoni alipingana na hoja hiyo.

Wengine walidai kwamba tatizo lilitokana na ‘stress’ za wakati wa mechi zilizoshtua baadhi ya mishipa anajibebesha mzigo mzito mno, uvumi na maneno havikuja na suluhisho ingawa bado dhana mbalimbali ziliendelea kuzungumzwa kuhusu tatizo hilo la Messi.

Mwezi huo huo, Barca wakapoteza taji la La Liga, huo ukawa msimu mbaya kwao, waliumaliza na taji moja tu, Spanish Super Cup. Messi anaweza kujivunia kuwa mfungaji bora wa wakati wote wa Barca lakini hilo halikuwa na maana kwa mchezaji wa hadhi yake ambaye amezoea kubeba mataji mengi.

Ni kama vile ulikuwa mfumo fulani, wakati Messi akiwa na wakati mgumu Ronaldo alikuwa akifurahia mafanikio yake uwanjani, msimu ulikuwa mzuri kwake, kati ya Septemba Mosi hadi Novemba 19 alifunga mabao yasiyopungua 34 katika mashindano yote humo humo zimo hat trick tano.

Lakini Ronaldo alichoonyesha zaidi ni umahiri katika kuzifumania nyavu, alikuwa amepevuka, mwenye kumudu maeneo yote na mtundu katika kuusoma mchezo.

Desemba 10 akiwa kwenye Uwanja wa Parken mjini Copenhagen, Denmark katika mechi ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, aliweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao tisa katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Hadi mwisho wa mwaka, Ronaldo akawa amefunga mabao 69 katika mechi 59 ikiwa ni uwiano wa wastani wa 1.16 ya mabao kwa kila mechi na huo ni ubora mwingine wa mchezaji huyo. Pamoja na rekodi hizo za kuvutia hakuweza kubeba taji la La Liga, ambalo msimu huo lilikwenda kwa Atletico Madrid wakati Real Madrid waliishia kwenye Kombe la Mfalme ambalo walilibeba Aprili 16, 2014 baada ya kuichapa Barca mabao 2-1.

Ni mechi ambayo Ronaldo hakucheza kutokana na kuwa na majeraha ambayo yamekuwa yakimuandama, tangu kuanza kwa mwezi Aprili, mwili wa Ronaldo ni kama vile ulianza kumpa dalili za kumwonya, madaktari waliompima walibaini matatizo makubwa ya misuli pamoja na goti la kushoto.

Madaktari hao wakapendekeza mchezaji huyo apumzike kwa hofu matatizo yangeweza kuwa makubwa, walisema kwamba mwili wa mchezaji huyo ulifikia hatua ambayo kilichohitajika ni pumziko.

Itaendelea Jumamosi ijayo….