Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabula afichua mambo matano, amtabiria Feitoto MVP

MABULA Pict

Muktasari:

  • Vitu hivyo ni ni kufanya mazoezi kwa bidii, kujitunza akimaanisha kula kwa wakati na kumpumzika pamoja na kunywa vinywaji nyenye virutubisho.

KIUNGO Mtanzania, Alphonce Mabula amesema anazingatia vitu vitatu muhimu ili kuwa na muendelezo wa kiwango bora uwanjani.

Vitu hivyo ni ni kufanya mazoezi kwa bidii, kujitunza akimaanisha kula kwa wakati na kumpumzika pamoja na kunywa vinywaji nyenye virutubisho.

Akizungumza na Mwanaspoti Mabula amesema huo ndio muongo wake wa maisha akiamini mchezaji anahitaji mambo hayo ili kuwa na kiwango bora uwanjani.

"Mfano wakati huu wa mapumziko mimi ratiba yangu nikiamka asubuhi nafanya mazoezi kisha nalala sana ili niweze kuuweka mwili vizuri na kunywa vinywaji vyenye virutubisho vinavyoujenga mwili," amesema Mabula.

MABU 01

Nyota huyo ambaye msimu uliopita aliachana na Shamakhi FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Azerbaijan baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kutamatika hivi karibuni.

Kwa sasa kiungo huyo yupo nchini mapumziko akisubiri ofa ya timu ambazo zinamuhitaji ikiwemo Kasimpasa S.K ya Ligi Kuu Uturuki ambayo iko kwenye mazungumzo na Mabula.

Licha ya kuwa mapumzikoni Mabula amesema anafuatilia Ligi Kuu Bara kwa sasa inavyoelekea mwishoni na ametoa mtazamo wake kuhusu nyota gani anaweza kuibuka Mchezaji bora wa msimu.

Mabula alimtaja kiungo wa Azam FC, Feisal Salum kuwa ndiye mchezaji bora wa msimu licha ya kwamba imesalia mechi moja tu ili ligi imalizike.

MABU 02

Mabula amesema Feitoto anastahili tuzo hiyo kutokana na mchango wake kwenye timu. Hadi raundi ya 29 nyota huyo anaongoza kwa ufungaji bora akiwa na mabao 15 na asisti nane.

"Ni mchezaji ambaye amepambana sana na ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa hata ukiwauliza wachezaji wa kigeni watamtaja Feitoto kwa sababu ya kiwango bora alichoonyesha."