Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabosi Simba wamgeukia Mudathir

Mabosi Simba wamgeukia Mudathir

KIUNGO wa zamani, Azam FC na Singida United, Mudathir Yahya ameingia kwenye rada za Simba ambao wapo sokoni kutafuta kiungo mpya wa ukabaji kutokana na kutolizishwa na ubora waliokuwepo sasa.

Inaelezwa mabosi wa Simba walifanya mawasiliano yenye usiri mkubwa na Mudathir ambaye kwa sasa ni mchezaji huru ila hakutoa majibu yoyote kama yupo tayari kujiunga na timu hiyo.

Mabosi hao wa Simba inaelezwa wanapambana na kutafuta kiungo mpya wa ukabaji huku, Afeez Nosiru kutokea Kwara United ya Nigeria ndio anapewa nafasi kubwa kama chaguo la kwanza kwenye usajili wa nafasi hiyo.

Mudathir kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Azam kuna nyakati aliwahi kueleza amepanga kupumzika kucheza mpira hadi dirisha dogo la usajili ndio atafanya maamuzi timu mpya ambayo atakwenda kuichezea.