Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzanite Manyara Marathon kuboresha huduma za afya kwa watoto njiti

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ameeleza hayo mjini Babati, leo Jumapili Agosti 9, 2026 kwenye mazoezi ya pamoja ya kuhamasisha jamii kushiriki mbio hizo.

Washiriki 1,500 tayari wameshajiandikisha kushiriki mbio za Manyara Tanzanite Marathon yenye lengo la kukusanya fedha za kuboresha huduma za afya kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao (njiti).

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ameeleza hayo mjini Babati, leo Jumapili Agosti 9, 2026 kwenye mazoezi ya pamoja ya kuhamasisha jamii kushiriki mbio hizo.

Sendiga amesema lengo ni kufikia washiriki 3,000 kwenye mbio za Tanzanite Manyara Marathon na sasa zaidi ya watu 1,500 wameajindikisha.

"Tunashukuru mwitikio ni mkubwa katika kujiandikisha kushiriki mbio hizo, watu mbalimbali wa Manyara na wengine kutoka nje ya Manyara wamejiandikisha kushiriki," amesema Sendiga.

Amesema mgeni rasmi katika mbio hizo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Lameck Nchemba, hivyo watu waendelee kujiandikisha ili washiriki katika jambo hilo.

Amesema wanatarajia kukusanya Sh1.5 bilioni kwenye mbio hizo kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa watoto njiti mkoani Manyara na wataanza na wilaya ya Hanang.

Amesema mbio hizo zimepangwa katika makundi tofauti hivyo watu wachague wenyewe kwani itahusisha kilomita tano, 10, 21 na 42.

Hata hivyo, amesema mazoezi ya kujiandaa na mbio hizo zitaendelea tena kwenye kila wilaya za Manyara, Agosti 15, 2026 yakiongozwa na wakuu wa wilaya.

Mmoja kati ya watu waliojiandikisha kushiriki mbio hizo, Frank Gidion, amepongeza jitihada za RC Sendiga za kukuza mchezo wa riadha na kuboresha sekta ya afya pamoja.

"Ewe mwana Manyara ambaye bado hujajisajili wakati ndiyo huu sasa, wekeza kwa ajili ya watoto wenye uhitaji maalum na Mungu wa mbingu na ardhi atakujazia pale ambapo umepapunguza kwa ajili ya kuwagusa hao watoto, ninaamini hakuna atakaye changia hili jambo Mungu akaacha kujibu mahitaji yake," amesema Frank.

Mshiriki mwingine, Magdalena Ombay, amempongeza RC Sendika kwa ubunifu kwani mkoa wa Manyara mchezo wa riadha ni nyumbani, hivyo mshale umerudi porini na watoto njiti watapatiwa vifaa pia.

"Mimi sijui viongozi wengine utendaji kazi wao ila kwa Manyara tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea RC Sendiga hapa Manyara," amesema Ombay.