Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabaharia waanza mwendo Ligi Kuu Zanzibar

KMKM Pict

Muktasari:

  • Kabla ya ushindi huo, mara ya mwisho timu hiyo ilipata ushindi wa mabo 2-1 dhidi ya Chipukizi kwenye fainali ya Kombe la FA iliyochezwa Juni 27, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba na kuwa wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

HATIMAYE mabaharia wa KMKM wamepata ushindi wa kwanza kwenye Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kuteseka kwa muda mrefu kwenye ligi hiyo.

Timu hiyo iliitandika JKU bao 1-0, mfungaji akiwa Abdul-Latif Shauri dakika ya 75 katika mchezo uliochezwa Septemba 30, 2026 kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

Kabla ya ushindi huo, mara ya mwisho timu hiyo ilipata ushindi wa mabo 2-1 dhidi ya Chipukizi kwenye fainali ya Kombe la FA iliyochezwa Juni 27, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba na kuwa wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

KMKM iliyoishia hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika ilipotolewa na Al Ahli Tripoli ya Libya kwa jumla ya mabao 7-0, imeanza Ligi Kuu Zanzibar kwa mwendo usioridhisha kufuatia kupoteza mechi tatu na sare moja kabla ya juzi kushinda kwa mara ya kwanza. Hadi sasa imeruhusu mabao sita kwenye mechi sita za ligi hiyo ikiwa ni wastani wa kuruhusu bao kila mechi. Ushindi huo umeifanya KMKM kupanda kutoka mkiani hadi kukamata nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Siyo jambo la kushangaza kwa timu hiyo kuanza vibaya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kwani kwa misimu ya hivi karibuni ikiwemo wa 2024-2025 na 2025-2026 haina tofauti na msimu huu.

Awali mabaharia hao walikuwa na timu yenye ushindani mkubwa ambapo ilitwaa ubingwa wa ZPL mara tisa na mwisho ilikuwa msimu wa 2022-2023 kabla ya kuvuliwa taji hilo na JKU msimu wa 2023-2024.

Licha ya kufanya vibaya ndani ya ligi, bado inaendeleza ubabe katika Kombe la FA kwani imechukua ubingwa mara mbili mfululizo 2024-2025 na 2025-2026 na kuwa wawakilishi kimataifa ingawa huishia hatua ya awali.

Matokeo ya mechi zingine zilizochezwa Septemba 30, 2026, kwenye Uwanja wa Annex kisiwani Pemba, Wembe ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mlandege, huku Chipukizi ikipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Zimamoto, mechi iliyochezwa Uwanja wa Gombani, Pemba.