Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKU yataja sababu ya kipigo ZPL

JKU Pict

Muktasari:

  • Kocha Mkuu wa JKU, Abdul-Saleh Mohammed amesema ukitoa ugumu wa mechi hiyo iliyochezwa Septemba 30, 2026 kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja, lakini bado safu ya ulinzi kwa timu hiyo haijawa imara ndio sababu ya kuruhusu mabao.

KATIKA kujiweka sawa na mbio za ubingwa Ligi Kuu Zanzibar, JKU imekatishwa spidi njiani kwa kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa KMKM huku lawama zote ikipewa safu ya ulinzi.

Kocha Mkuu wa JKU, Abdul-Saleh Mohammed amesema ukitoa ugumu wa mechi hiyo iliyochezwa Septemba 30, 2026 kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja, lakini bado safu ya ulinzi kwa timu hiyo haijawa imara ndio sababu ya kuruhusu mabao.

“Safu ya ulinzi bado changamoto upande wetu ndio maana tunafungwa, lakini najaribu kurekebisha makosa tutakaa sawa,” amesema.

Pia kocha huyo amebainisha kwamba, ukiweka kando ishu ya safu ya ulinzi, wachezaji wa kikosi hicho walizidiwa mbinu na wapinzani, hali iliyowapa KMKM nafasi ya kufunga bao pekee la ushindi.

Alikiri kuwa, mchezo huo ulikuwa mgumu na tofauti na walivyotarajia kwani wapinzani wao walijipanga vyema na kuonesha umakini wakati wote wa mchezo wakihitaji ushindi.

Kocha huyo amebainisha kwamba kulikuwa na changamoto ya umaliziaji kwa baadhi ya wachezaji na wanaendelea kuifanyia kazi ili kuhakikisha wanapata mabao katika nafasi wanazotengeneza.

Licha ya kupoteza mchezo huo, kocha huyo amesisitiza kuwa hawajakata tamaa katika mbio za ubingwa kwani ligi bado ni ndefu na kuna michezo mingi mbele yao.

Timu hiyo itashuka tena dimbani Oktoba 4, 2026 ikichuana na Uhamiaji kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

Kipigo hicho cha kwanza kwa JKU kwenye ligi hiyo msimu huu, kimeifanya kushika nafasi ya tano katika msimamo ikiwa na pointi nane ikicheza mechi tano. Hiyo ni kabla ya mechi mbili za leo.