Lusajo, Mhilu kuiongoza Tanzania

WACHEZAJI Reliants Lusajo na Yusuph Mhilu ni miongozi mwa wachezaji 11 waliochaguliwa na kocha mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Sudani Kusini, kwenye mchezo unaofanyika katika uwanja wa Bahir Dar, Nchini Ethiopia kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) U-23.
Kikosi kinachoanza ni Wilbol Maseke, Nickson Kibabage, Lusajo Mwaikenda, Sospeter Israel, Meshack Abraham, Reliants Lusajo, Kelvin Noshan, Abdulrazack Mohammed, Yusuph Mhilu, Andrew Simchimba, na Israel Patrick.
Wachezaji wa akiba ni Daniel Mgore, Aman Haji, Oscar Masai, Lucas Kikoti, Joseph Mkele, Rajab Hassan, Erick Mwijage, Abdulmajid Mangalo na Pascal Msindo.
IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI