Lukuvi aenziwa Mkutano Mkuu wa Yanga
Muktasari:
- Lukuvi aliyekuwa Mbunge wa Isimani, Mkoa wa Iringa, kuanzia mwaka 1995, akihudumu kwa miaka 30, alifariki dunia Machi 25, 2026, kwa mshtuko wa Moyo, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
ALIYEKUWA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi, ameenziwa katika Mkutano Mkuu wa Yanga, unaofanyika leo Jumapili ya Agosti 2, 2026, kwenye Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.
Lukuvi aliyekuwa Mbunge wa Isimani, Mkoa wa Iringa, kuanzia mwaka 1995, akihudumu kwa miaka 30, alifariki dunia Machi 25, 2026, kwa mshtuko wa Moyo, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Katika mkutano wa leo, mbali na Lukuvi, wanachama wengine wa Yanga walioenziwa ni Yusuph Mwandami, Stephen Hyera, Samson Mwakalinga, Damian Kinyunyu, Kulwa Mussa, Rajabu Selemani, Musa Monde, Eddah Mkama, Andrew Msolo, Kanyika Mshana, Beatus Linda, Adventina Mwanamaya, Saidina Amani, John Makotta, Alex Msamba, Ramadhani Ramadhani, Ruya Fumbogoro na Athumani Puga.
Yanga inafanya mkutano wake mkuu leo Jumapili ya Agosti 2, 2026, kwenye Ukumbi wa The Super Dome, ukiwa na ajenda 14, huku miongoni mwa hizo ni Uchaguzi Mkuu wa kuwachagua, Rais, Makamu wa Rais na wajumbe watano watakaounda Kamati ya Utendaji kwa miaka minne ijayo kuanzia sasa.