Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luis aachana na Ahly, Simba washindwe wenyewe

Muktasari:

  • Uamuzi huo umefikiwa wakati winga huyo akirejea kwenye klabu hiyo akitokea Abha FC ya Saudi Arabia alikokuwa akicheza kwa mkopo.

WINGA wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Al Ahly ya Misri na sasa ni mchezaji huru, imeripotiwa.

Uamuzi huo umefikiwa wakati winga huyo akirejea kwenye klabu hiyo akitokea Abha FC ya Saudi Arabia alikokuwa akicheza kwa mkopo.

Luis alijiunga na miamba hiyo ya soka ya Misri akitokea Simba ya Tanzania miaka miwili iliyopita.

"Ningependa kushukuru uongozi wa klabu, wachezaji wenzangu na makocha niliyofanya nao kazi mahali hapa. Ningependa pia kuwashukuru mashabiki wa Al Ahly," amesema Luis.

Winga Luis amekuwa akihusishwa na mpango wa kurudi kukipiga kwenye timu yake ya zamani ya Simba yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi kwenda kuchukua nafasi ya Peter Banda

Wekundu Msimbazi hao kwa sasa wapo zao Uturuki wakijifua kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.