Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa Sugar yaachana na Chippo

CHIPPO Pict

Muktasari:

  • Chippo anakumbukwa na mashabiki wengi hasa baada ya kukiongoza kikosi cha Ulinzi Stars kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu ya Kenya ‘KPL’ kati ya 2003 na 2005 na kuhudumu akiwa kocha msaidizi wa Harambee Stars kuanzia 2008 hadi 2011.

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umefikia makubaliano ya kutoendelea na aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Mkenya Yusuf Chippo baada ya kuishuhudia timu hiyo ikishuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara hadi Championship kwa msimu uliopita wa 2025-2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha huyo wa zamani wa Pamba Jiji, Coastal Union na TRA Unit-ed zamani Tabora United, amesema wamefikia makubaliano ya kutoendelea na kikosi hicho kwa msimu wa 2026-2027, kutokana na mambo mbalimbali yaliyotokeza.

“Tumefikia makubaliano ya kutoendelea na Mtibwa Sugar na sasa nimerudi kwetu Kenya, msi-mu wa 2025-2026, ulikuwa ni mgumu sana kwangu kwa sababu sikutegemea kabisa ningeku-wa pia miongoni mwa sehemu ya kuishusha timu daraja,” amesema Chippo.

Kocha huyo amesema licha ya timu hiyo kushuka daraja ila anaamini bado itarejea tena Ligi Kuu Bara kutokana na aina ya wachezaji waliopo, japo malengo yake makubwa yalikuwa ni kuendelea kuipigania kwa lengo la kuirudisha sehemu iliyokuwa.

Chippo aliyeachana na Murang’a SEAL ya kwao Kenya tangu Agosti 21, 2025, alijiunga na timu hiyo kwa ajili ya kuiongoza msimu wa 2025-2026, akishirikiana na Awadh Juma ‘Maniche’ ali-yeipandisha daraja kwenda Ligi Kuu kwa msimu wa 2024-2025.

Kocha huyo alijiunga rasmi Mtibwa Sugar, Novemba 17, 2025 na kwa msimu wa 2025-2026, alimaliza nafasi ya 15 na pointi 27 katika Ligi Kuu na kikosi hicho kushuka daraja na KMC FC ili-yomaliza mkiani na Tanzania Prisons iliyoshuka kwa Play Off.

Chippo anakumbukwa na mashabiki wengi hasa baada ya kukiongoza kikosi cha Ulinzi Stars kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu ya Kenya ‘KPL’ kati ya 2003 na 2005 na kuhudumu akiwa kocha msaidizi wa Harambee Stars kuanzia 2008 hadi 2011.