Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi ya Viziwi Zanzibar kuhitimishwa kesho

VIZIWI Pict

Muktasari:

  • Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 2, 2026 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Michezo ya Viziwi Zanzibar (SHIMIVIZA).

FAINALI ya Ligi ya Viziwi Zanzibar kati ya Hope Deaf City na Wakombozi, itachezwa kesho Jumamosi jioni, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 2, 2026 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Michezo ya Viziwi Zanzibar (SHIMIVIZA).

Akitoa taarifa hiyo, Ofisa Habari na Mawasiliano  ZFF, Namala Suleiman, amesema ligi hiyo itaanza kuchezwa saa nane kati ya Zan Deaf na Vuka City kutafutwa nafasi ya tatu, huku fainali ikichezwa saa 10 jioni kutafuta mshindi.

VIZI 01

"Fainali ya Ligi ya Viziwi itachezwa kesho, hivyo tunawaomba mashabiki wafike uwanjani kuwapa hamasa kama ilivyo mechi nyingine," amesema.

Amefafanua kuwa, ligi hiyo ni miongoni mwa mipango ya ZFF kusimamia soka la watu wenye ulemavu, hivyo ndio sababu kubwa ya kuanzishwa kwake.

Naye Katibu wa SHIMIVIZA, AbdulAzizi Mohammed Mahfoudh, amelishukuru Shirikisho hilo kukubali kuwaunga mkono na kuwapa fursa ya kuonesha vipaji vyao.

VIZI 02

Amesema baada ya mashindano hayo yaliyoshirikisha timu nne, zimejitokeza timu 12 kushiriki kwenye ligi hiyo kupata wachezaji watakaoiwakilisha Zanzibar kimataifa.

AbdulAzizi amesema wapo wachezaji wengi viziwi wenye vipaji vya namna hiyo lakini walikuwa hawajui sehemu ya kuvionesha.

Hivyo, kuanzishwa kwa ligi hiyo itawapa nafasi ya kuvionesha na watu kufurahia soka la viziwi.