Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi ya viziwi yazidi kunoga Zanzibar

VIZIWI Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyochezwa Septemba 18, 2026 kwenye Uwanja wa Mao B, Unguja, Ibrahim Iddi aliitangulizia Wakombozi kwa bao la dakika ya 29, kabla ya Ali Hassan kuisawazishia Vuka dakika ya 56.

LIGI ya Viziwi Zanzibar, imeendelea kushika kasi kisiwani hapa, baada ya mchezo kati ya Vuka na Wakambozi kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mechi hiyo iliyochezwa Septemba 18, 2026 kwenye Uwanja wa Mao B, Unguja, Ibrahim Iddi aliitangulizia Wakombozi kwa bao la dakika ya 29, kabla ya Ali Hassan kuisawazishia Vuka dakika ya 56.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Kocha wa Vuka, Haji Kombo amesema baada ya kutanguliwa kwa bao moja, hamasa ya timu ilishuka.

DE 01

Aliema, wakati timu hizo zilipokwenda mapumziko, aliamua kufanya mabadiliko kwa kuongeza wachezaji wenye kasi kwa lengo la kuipa uhai timu.

“Kwenye mechi ya marudio naamini tutafanya vizuri, viziwi tunaweza na tunafurahi sana kupata nafasi hii, tunaoimba Serikali iendelee kutushika mkono,” amesema.

Kocha huyo amesema kwenye timu hiyo aliona changamoto kubwa ilikuwa wachezaji wanapasia zaidi kuliko kushambulia.

DE 02

Alieleza wachezaji wake walikuwa wakifika langoni la mpinzani, badala ya kufunga wanarudisha mipira nyuma, hivyo, watafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza kwenye mechi hiyo.

Ligi hiyo iliyoanza Septemba 17, 2026, inashirikisha timu nne na itachezwa kwa siku kumi ili kupata wachezaji wa timu ya taifa ya viziwi kwa ajili ya mashindano ya kimataifa yatakayofanyika nchini Ethiopia.