Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu kilio cha wadau Iringa

IRINGA Pict

Muktasari:

  • Hii ni kutokana na kusuasua kwa matokeo ya TMA inayoshiriki Championship ikiwa mkiani kwa pointi mbili na kukatisha tamaa katika hesabu za kupata timu ya Ligi Kuu.

MWENENDO wa soka mkoani Iringa umewashtua wadau wakiomba juhudi binafsi za wadau na serikali kuungana pamoja kunusuru vipaji vya vijana.

Hii ni kutokana na kusuasua kwa matokeo ya TMA inayoshiriki Championship ikiwa mkiani kwa pointi mbili na kukatisha tamaa katika hesabu za kupata timu ya Ligi Kuu.

Iringa haijaonja ladha ya Ligi Kuu kwa misimu mitano tangu Lipuli 'Wanapaluhengo' iliposhuka daraja huku juhudi za kupata mbadala zikionekana kutokuwa mafanikio katika soka.

Tangu iliposhuka Lipuli, baadhi ya wadau wakishirikiana na Halmashuri waliinunua Ruvu Shooting lakini haikuwa na maisha marefu na kujikuta ikipoteana na sasa macho yote yapo kwa TMA.

Felix Mzava amesema kwa sasa vipaji vya vijana viko shakani kutokana na kukosa muelekeo akieleza kuwa namna ya kusaidia kundi hilo ni ushirikiano wa wadau na serikali ya Mkoa kupata timu.

Amesema mpira umekuwa chachu ya maendeleo kwa vijana ukifungua fursa za uchumi na ajira, hivyo ili kuinua na kuendeleza soka kuwepo vituo vya kukuza badala ya kununua timu.

"Kuwepo nguvu ya wadau wakishirikiana na serikali kurengeneza timu moja ya hapahapa Iringa badala ya kununua ambayo imeshafika hatua za juu, huu si uzalendo"

"Hata vituo vya kulea na kukuza vipaji 'Academy' ni chache sana ukilinganisha na idadi ya vijana wanaocheza mpira, hii inazorotesha maendeleo ya Mkoa" Amesema Mzava.

Naye Erick Vicent aliyewahi kucheza timu ya vijana (U20) ya Lipuli amesema tangu kushuka kwa timu hiyo imepoteza muelekeo wa kipaji chake na ndoto za kucheza mpira akikiri uwapo wa athari ya kutokuwa na timu za ushindani.

"Dar es Salaam vipaji ni vichache lakini kwa kuwa kuna timu nyingi ndio maana vijana wengi wanakimbilia huko kutafuta fursa, lakini mikoani uwezo wetu ni mkubwa" amesema Vicent.