Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Morrison zege halilali

KAMA unaendelea kumchukulia poa winga mtata wa Simba, Bernard Morrison ‘BM3’ pole yako, kwani jamaa amesema kwake zege halilali.

Winga huyo aliyesajiliwa kutoka Yanga, alisema kwa sasa hataki maneno mengi, bali anaicha miguu yake izingumze zaidi uwanjani na kuwajibu wale wote wanaochonga juu yake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Morrison ambaye amekuwa hana nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza tangu asajiliwe msimu huu akitokea Yanga, huku akiwa kipenzi cha mashabiki wa Jangwani, alilisisitiza kwake kazi inaendele na hana muda na maneno.

“Naamini kufanya kazi kwa bidii, ndio maana sipendi kuongea, napenda kujituma ili kazi yangu ndio iongee zaidi. Huu ni wakati wa kuwajibika ipasavyo kuisaidia timu kutetea ubingwa na kuwafurahisha mashabiki wetu kama tutafikia malengo yetu ambayo wanayatazamia kutoka kwetu,” alisema winga huyo Mghana mwenye mabao matatu mpaka sasa katika Ligi Kuu Bara.

Mbali na hilo aliwahamasisha wachezaji wenzake kupiga kazi hasa kipindi hiki chenye ushindani mkali unaotokana na baadhi ya timu zinazojilinda zisishuke daraja na zile zinazowania taji la ligi hiyo.

“Jambo la msingi ni pointi tatu zitakazotokana na kujituma na kujitolea, ili kufikia malengo ya kutetea taji hilo, itakuwa mara ya nne kama tutafanikisha,” alisisitiza nyota huyo wa zamani wa AS Vita ya DR Congo.

Kuhusu pambano la watani litakalochezwa Mei 8, kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam alijibu kwa kifupi kwamba kwa mwonekano wake wa kufuga ndevu nyingi unafanana na Simba, hivyo mechi hiyo haitakuwa ya kitoto siku hiyo.

“Sitaki kulizungumzia hilo, ila mwonekano wangu kwa sasa nimekaa kama Simba, hilo linatosha kudhihirisha itakuwa ni mechi ya aina gani, tusubiri siku ifike ndo mtajua namaanisha nini.”