Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KVZ, UhamiajI zashindwa kutambiana

KUTAMBIANA Pict

Muktasari:

  • Sare hiyo imeifanya KVZ kushindwa kuongeza pengo la pointi dhidi ya Uhamiaji, ambayo nayo inaendelea kuwania nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo.

TIMU za KVZ na Uhamiaji FC zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliochezwa kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

Matokeo hayo yameifanya KVZ kufikisha pointi 18 na kuendelea kushikilia nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo, huku Uhamiaji ikifikisha pointi 16 na kubaki katika nafasi ya tano.

Sare hiyo imeifanya KVZ kushindwa kuongeza pengo la pointi dhidi ya Uhamiaji, ambayo nayo inaendelea kuwania nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Novemba 6, 2026, Zimamoto iliisulubu Black Sailors kwa kuifunga mabao 2-1 na kufanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 25.

Kipigo hicho kimeifanya Black Sailors kuendelea kusalia katika nafasi ya 13 ikiwa na pointi tisa, huku ikiwa miongoni mwa timu zilizo katika hatari ya kushuka daraja msimu huu.

Wakati huo huo, sare ya Polisi dhidi ya KMKM imeifanya timu hiyo kupunguza kasi katika mbio za kuwania nafasi ya juu, ikiendelea kubaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22, tofauti ya pointi tatu na vinara Zimamoto.