Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KVZ na mikakati ya kutetea ubingwa

KVZ Pict

Muktasari:

  • KVZ ilitwaa taji la ligi hiyo msimu wa 2025-2026 kwa kukusanya pointi 67. Hata hivyo, msimu huu haijaanza kwa kasi iliyotarajiwa, baada ya kucheza michezo saba, kushinda minne, kutoka sare moja na kupoteza miwili.

OFISA Habari na Mawasiliano wa KVZ, Abduljalil Mohamed Salum amesema timu hiyo inalenga kushinda michezo iliyosalia katika mzunguko wa kwanza ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake.

KVZ ilitwaa taji la ligi hiyo msimu wa 2025-2026 kwa kukusanya pointi 67. Hata hivyo, msimu huu haijaanza kwa kasi iliyotarajiwa, baada ya kucheza michezo saba, kushinda minne, kutoka sare moja na kupoteza miwili.

Matokeo hayo yameifanya KVZ kukusanya pointi 13 na kushika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo.

Abduljalil amesema kwa sasa timu hiyo inaweka mkazo zaidi katika kupata matokeo mazuri kutokana na ushindani mkubwa uliopo katika ligi ya msimu huu, ambayo inahitaji umakini katika kila mchezo.

Amesema licha ya kutokuwa kileleni mwa msimamo, KVZ bado ina nafasi ya kufanya vizuri na kutimiza lengo lake la kutetea ubingwa.

“Msimu wa 2024-2025 tuliwahi kukosa ubingwa kwa tofauti ya mabao, kwa hiyo hatutaki kurudia makosa. Ndiyo maana tunataka kushinda kwa mabao mengi katika kila mechi,” amesema. Abduljalil aliwaomba mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuiunga mkono kwa kuwa uwepo wao huwapa wachezaji hamasa na nguvu ya kupambana kutafuta matokeo mazuri.

Alisisitiza kuwa ushindi wa ligi ni jambo muhimu kwa timu hiyo, ndiyo maana mikakati yao ni kuhakikisha inashinda michezo yote iliyosalia ili kuongeza nafasi ya kutetea taji lake.