Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Depu aipa mkwanja mrefu Yanga


YANGA imeshafika hatua za mwisho kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wake, Laurindo Aurelio ‘Depu’, baada ya kupokea ofa nzuri kutoka klabu ya Petro Atletico ya Angola inayotaka kumsajili katika dirisha hili kuelekea msimu ujao wa 2026-2027.


Mwanaspoti linafahamu kuwa, viongozi wa Yanga wameshapokea ofa hiyo na tayari wameruhusu nyota huyo kuondoka kutokana na makubaliano ya mwisho kukamilika kwa pande zote mbili.

Yanga imemuuza Depu akiwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na nusu, baada ya kuichezea klabu hiyo kwa nusu msimu, huku akiacha rekodi ya kufunga jumla ya mabao 14, Ligi Kuu akiwa na tisa na asisti mbili, wakati FA akipachika matatu na Ligi ya Mabingwa mawili.

Mwanaspoti linafahamu kuwa, Yanga itavuna kiasi cha Sh1.1 bilioni kwa kumuuza Depu kwenda Petro Atletico ya kwao Angola, huku taarifa zikieleza kila kitu kimeshakamilika na mshambuliaji huyo anajiandaa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya, kisha kusaini mkataba na Waangola hao.

“Depu kwa sasa anajiandaa na safari ya kurejea Angola ili kukamilisha mchakato wa uhamisho wake kwa kujiunga na klabu hiyo lakini kwanza atafanyiwa vipimo,” kilisema chanzo.

Wakati huo huo, mabingwa hao mara tano mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara tayari wameshapata mtu wa kuchukua nafasi ya nyota huyo wa kimataifa kwa kufanya kumsajili beki raia wa Ivory Coast, Oumar Farouk Komara, aliyekuwa akikipiga Golden Arrows ya Afrika Kusini.

Taarifa za ndani zilisema kocha Manqoba Mngqithi amehusika moja kwa moja katika kumpendekeza Komara kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja, jambo ambalo linaonekana kuwa muhimu katika mipango ya kiufundi ya timu hiyo kuelekea msimu mpya.

Chanzo kilisema ujio wa Komara una faida kubwa kwa Yanga, hasa katika kipindi hiki ambacho beki wa kati, Dickson Job, bado hajarejea rasmi uwanjani baada ya kusumbuliwa na majeraha tangu msimu uliopita.

“Komara ni chaguo la benchi la ufundi. Ana uwezo wa kucheza beki na pia kiungo mkabaji, hivyo atatoa suluhisho kwenye maeneo mawili muhimu ndani ya kikosi,” kimesema chanzo hicho.

Mbali na kucheza kama beki, Komara pia ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, jambo litakalompa kocha Manqoba chaguo zaidi katika kupanga kikosi kulingana na mahitaji ya kila mechi.

Usajili wa Komara na kuondoka kwa Depu, unafanya Yanga kuwa na idadi ya wachezaji 12 wa kigeni wanaotakiwa kikanuni ambao ni Komara, Fred Ngoma, Cheikh Ibrahima Touré, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, Peter Shalulile, Djigui Diarra, Kouassi Attohoula Yao, Chadrack Boka, Duke Abuya, Maxi Mpia Nzengeli na Allan Okello.