Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kutoka Simba hadi Yanga, Mwalimu awaingizia Wydad mamilioni


UHAMISHO wa mshambuliaji wa Kitanzania, Selemani Mwalimu ‘Gomez’ kwenda Yanga kwa mkopo umeifanya Wydad Athletic Club ya Morocco kuvuna mkwanja mrefu, licha ya mchezaji huyo kutokuwa sehemu muhimu ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


Mwalimu alijiunga na Yanga kwa mkopo wa msimu mmoja, katika dili linalotajwa kuwa na thamani ya Dola 200,000 (Sh500 milioni), ikiwa ni sehemu ya mapato ambayo Wydad imeendelea kuyapata kutokana na kumiliki haki za mchezaji huyo aliyejiunga nayo mwaka 2025 akitokea Fountain Gate kwa mkataba wa miaka minne na nusu.

Wydad ilimsajili Mwalimu kutoka Fountain Gate kwa ada ya Dola 150,000 (Sh397 milioni).

Baada ya usajili huo, klabu hiyo imeendelea kunufaika kifedha kutokana na mikataba ya mkopo ya mshambuliaji huyo.

Mwalimu ambaye alitengeneza jina lake Tanzania akiwa Fountain Gate, msimu uliopita alicheza kwa mkopo Simba baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza Wydad.

Simba ililipa Dola 50,000 (zaidi ya Sh130 milioni) ili kupata huduma yake hatua iliyompa Mwalimu nafasi ya kurejea nchini na kuonyesha uwezo wake Ligi Kuu Bara.

Sasa Mwalimu ameibukia Yanga baada ya umafia uliofanywa na Injia Hersi Said baada ya watani zao kushindwa kukamilisha dili hilo kwa wakati, ikumbukwe mshambuliaji huyo alikuwa kwenye mipango ya Simba msimu huu.

Kitendo cha Yanga kutoa Dola 200,000 kwa ajili ya mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo kwa Mwalimu, dili hilo limekuwa na faida.

Hadi sasa klabu hiyo imevuna mamilioni ya mikataba miwili tofauti ya mkopo, kwanza kutoka Simba iliyolipa Dola 50,000 zaidi ya Sh130 milioni, kisha Yanga iliyolipa Dola 200,000 zaidi ya sh500 milioni, ikiwa tayari ina faida ya Dola 100,000 huku mchezaji huyo akiwa na mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo.

Kwa maana hiyo, Mwalimu ameendelea kuwa na thamani kubwa kibiashara, akisaidia klabu hiyo kurejesha fedha aliyosajiliwa kutokana na mikataba yake ya mikopo pamoja na faida kubwa.

Akiwa Simba msimu uliopita, Mwalimu alifunga mabao tisa ligi kuu, akivunja rekodi yake binafsi ya mabao aliyowahi kufunga msimu mmoja wa ligi pia aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano alipopachika bao moja dhidi ya Yanga.

Kabla ya hapo, katika msimu wake wa kwanza kucheza Ligi Kuu akiwa Fountain Gate, Mwalimu alifunga mabao sita kabla ya kujiunga na Wydad.